• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Itigi awataka Madiwani na Watumishi kufanya Kazi kwa ushirikiano kukidhi Mahitaji ya wananchi.

Tarehe ya Kuwekwa: December 16th, 2020

Na Luganuzi Muwelu.  H/W-ITIGI

Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Mh, Hussein Ibrahimu Simba Ambaye pia ni Diwani wa kata ya Tambukareli Amesema kuwa Waheshimiwa  Madiwani na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Itigi wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa

ili kukidhi na kutoa huduma bora kwa wananchi. Mh Simba amesema kuwa Wananchi hawa wanategemea huduma bora na hawahitaji migogoro kati ya Mh Diwani na Mtendaji

Aidha Mh.Simba Amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo  Bw  John K. Mgalula kwa kusimamamia ukusanyaji mzuri wa mapato ya ndani pamoja  Mweka hazina wa Halmashauri  Hiyo Bi Neema Lumambo kwa kuwa mipango mizuri ya ukusanyaji na ufuatiliaji mzuri wa Mapato hayo ambapo hapo Awali makusanyo ya ndani yalikuwa kidogo tofauti na sasa ambapo Makusanyo ni zaidi ya Million 100  kwa Mwezi.

Mh Simba pia amewataka Waheshimiwa Madiwani kwenda kusimamia upungufu wa Madawati Katika shule zao na Wanafunzi wote ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanakwenda shule na  kushirikiana na Watendaji kuchukua hatua kwa Wazazi watakaobainika kuwazuia watoto waliofaulu kutokwenda shule kwa namna moja ama nyingine.

Aidha Simba ametoa shukrani kwa Waheshimiwa madiwani wote kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo ya kuongoza halmashauri kwa nafasi ya uenyekiti wa halmashauri kwa miaka mitano na kuahidi ushirikiano mkubwa kati yake na Madiwani, Wananchi na Watendaji wote wa Serikali katika lengo moja tu la kuwatumikia wananchi na kuhakikisha huduma bora zinazotakiwa kutolewa zinatolewa.

Nae   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi  Bw. John K. Mgalula amesema kuwa yeye kama katibu wa baraza la Madiwani ataendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha shughuli zote za serikali zinafanyika kwa ukamilifu wake

Katika hatua Nyingine Mkuu wa Wilaya ya Manyoni na Mgeni Rasmi Bi Rahab Mwangisa amewataka Waheshimiwa Madiwani kuwa daraja kati ya Wananchi na Serikali na kuhakikisha changamoto ambazo zinawakabili wananchi zinatatuliwa kwa wakati .  

Aidha Mh Mkuu wa Wilaya Amewataka Madiwani kwenda kuhamasisha  wananchi ujiungaji wa mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa  ambayo itawasaidia wananchi hao kupata Matibabu kuanzia ngazi  Zahanati   mpaka Hospitali ya Mkoa kwa Kiasi cha Sh 30,000 tu kwa kila Kaya. Mwangisa Amesema  kuwa ni vizuri kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya  ili wananchi wahamisike kujiunga ambapo itawasidia katika suala zima la Matibabu pale mmoja wa familia anapoumwa

Awali uchaguzi wa ulifanyika wa kumchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi na Kupelekea Mhe Diwani wa Tambukareli Husseni Simba Kuibuka Mshindi Kwa kupata kura 18 za Ndio na Kura 1 ya hapana na kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya  Itigi na Makamu Mwenyekiti Mhe. Diwani wa Kata ya Mwamagembe  Jonathan Dulle Kuibuka Mshindi kwa kupata kura 16 za ndio na Kura 3 za hapana.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 December 15, 2018
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili September 12, 2017
  • TANGAZO LA UUZAJI WA MAGOGO February 28, 2018
  • Tangazo la Zabuni July 02, 2018
  • Tazama zote

Habari mpya

  • Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Itigi awataka Madiwani na Watumishi kufanya Kazi kwa ushirikiano kukidhi Mahitaji ya wananchi.

    December 16, 2020
  • TASAF KIPINDI CHA PILI AWAMU YA TATU HALMASHAURI YA ITIGI YAANZA NA UHAKIKI WA KAYA

    August 01, 2020
  • MGANGA MKUU ITIGI DR MALLANGE AENDELEZA OPERATION FUNGIA MAABARA BUBU

    February 04, 2020
  • Mganga Mkuu Itigi Dr. Mallange azifungia Maabara mbili kwa kukiuka utaratibu

    November 12, 2019
  • Tazama zote

Video

RAIS MAGUFULI AADHIMISHA SIKU YA MASHUJAA ITIGI SINGIDA NA WANANCHI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0737235630

    Simu ya Mkononi: 0757226612

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa