• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

ALMASI YA ITIGI NI PAMBA; MWANRI

Posted on: October 16th, 2022

Wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi wameshauriwa kulima zao la pamba kama miongoni mwa mazao ya biashara kwa kuwa jografia yake inaruhusu zao hilo kustawi.

Akizungumza na wanachi katika ziara maalumu katika halmashauri hiyo  iliyoanza tarehe 13-14 Oktoba 2022 ya kuhamasisha kilimo cha zao la pamba Balozi wa pamba Tanzania Ndg.Agrey Mwanri amesema  halmashauri ya Itigi ina eneo kubwa na zuri kwa ajili ya kilimo na hususani kilimo cha pamba kwa kuwa zao hilo linahitaji mvua za wastani ambazo ni asilimia hamsini(50%) ya mvua zinazonyesha  katika mikoa ya kanda ya kati.

Amesema kuwa Mkoa wa Singida umepitisha azimio kua kila mwananchi kwa kuanzia alime angalau heka moja ya zao la pamba huku akibainisha kuwa serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Samia Suluhu Hassani rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshatoa mbolea za ruzuku sanjari na pembejeo nyingine kama mbegu na viuatilifu ambavyo wakulima watapatiwa kwa mkopo kupitia Bodi ya pamba (TCB).

Aidha Mwanri amesema kuwa  serikali imeandaa soko la uhakika la pamba kwa bei elekezi  ya Tsh 1600 kwa  kilo huku makampuni mengine yanayonunua pamba  ikiwemo  Bio Sustain Tanzania Limited wananunua pamba kwa ts, 2000 kwa kilo na kuwataka wananchi  wa halmashauri ya Itigi kuchangamkia fursa hiyo.

Kwa upande wake Afisa kilimo wa halmashauri ya Wilaya ya Itigi Bw. Mkinguzi Mgalula amesema Halmashauri imejipaga kutekeleza mpango huo kwa kuwasaidia wakulima waweze kulima kilimo cha kisasa cha zao la pamba ili waweze kupata tija .

Nae Bi Maria Mtonyi mkazi wa kijiji cha Gurungu na Bw. Herman Sifuni wameshukuru serikali kwa  kwa kupatiwa semina hiyo kupitia kwa Balozi wa pamba nchini Ndg. Agrey Mwanri na kwamba imeamsha ari ya kulima zao hilo ambalo kwa kiasi kikubwa wananchi wa maeneo hayo walishakata tama kutokana na changamoto mbalimbali zilizokuwepo ikiwemo ukosefu wa soko la uhakika .

Ziara hiyo katika halmashauri ya Itigi imehusisha vijiji sita ikiwa ni pamoja na  Idodyandole,Mwamatiga,Makuga ,Doroto,Kashamawele na Gurungu.

Mwisho

Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.