• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

MGOGORO MRADI WA MAJI, KIHANJU WAPATA MWAROBAINI

Tarehe ya Kuwekwa: March 18th, 2022

                     

Kikundi cha umoja wa Wajasiriamali Tarafa ya Itigi (UWATI) kimekubali kushirikiana na Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) kutekeleza mradi wa maji katika kijiji cha Kihanju,Halmashauri ya Itigi kwa lengo la kutatua kero ya uhaba wa maji kwa matumizi ya kawaida pamoja na kilimo cha umwagiliaji.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika kikao cha maridhiano  baina ya pande hizo mbili  kilicho fanyika katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Itigi baada ya kikundi cha UMATI  kudai kuwa RUWASA wamewanyang’anya mradi  walioumba kufadhiliwa na kampuni ya vinywaji ya  Serengeti (SBL) kwa lengo la kikundi hicho kufanya kilimo cha umwagiliaji cha zao la vitunguu.

Akitoa taarifa ya mradi  Eng. Maduhu kutoka RUWASA  wilaya ya Manyoni ameeleza kuwa mradi huo uliibuliwa na kikundi cha UMATI mwaka 2021 na kuandika andiko la kuomba msaada wa kujengewa miundombinu ya umwagiliaji pamoja na kisima katika eneo la mradi wao wa kilimo cha umwagiliaji  ambapa Kampuni ya vinywaji ya Serengeti(SBL) lilikubali kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni mia mbili(Tsh mil.200) kupitia Shirika la WaterAid Tanzania ili kutekeleza mradi huo

Aidha baada ya upembuzi yakinifu WaterAid,RUWASA mkoa Singida  na wilaya ya Manyoni pamoja na wadau mbalimbali wa maji walibaini uhaba wa maji kwa wakaazi wa Kihanju na kuamua kutoa kipaembele kwa wananchi kama sera ya maji ya mwaka 2002 inavyoelekeza ambapo jambo hilo liliibua hisia tafauti kwa kikundi cha UMATI .

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mipango na Usimamizi  wa Miradi ya WaterAid Tanzania  Dkt.Nduhura Innocent ameishauri serikali  kupitia Halmashauri kutoa elimu kwa wana kikundi cha UMATI  kuelewa faida ya mradi huo kwa  jamii badala ya kuibua migogoro inayoweza kupelekea wadau kushindwa  kufadhili miradi mingine katika Halmashauri ya Itigi.

Naye Mjumbe wa UMATI Bw. Omari Malele amesema kuwa  kikundi kimeridhia mradi uendelee lakini kuwepo na ushirikishwaji  kwa kuwa kikundi hicho ndio kilichoibua huo mradi huku Kaimu Katibu wa UMATI Bw.Hamisi Samade  amewashukuru wajumbe kutoka WaterAid kwa kuja kutatua mgogoro uliokuwepo baina ya pande hizo mbili.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi Mh. Hussein Simba akafafanua jinsi mchakato mzima wa uanzishwaji wa mradi ulivyokua shirikishi na kusema kuwa jamii  pamoja na kikundi cha UMATI wanapaswa kuchangia huduma ya maji  ili mradi huo uweze kujiendesha.

Usanifu wa Mradi wa maji wa Kihanju ulianza mwezi julai ,2021 na utekelezaji wake ukaanza mnamo Disemba 2021 na unatarajiwa kutosheleza mahitaji ya maji ya watu zaidi ya 2000 katika kijiji hicho na maeneo ya jirani.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa