• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

Migogoro ya Wakulima na Wafugaji Wilayani Manyoni yapatiwa mwarobaini

Tarehe ya Kuwekwa: October 6th, 2017



MKUU WA WILAYA AKEMEA VIKALI VIASHIRIA VYA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI ITIGI


Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekemea vikali viashiria vya mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika maeneo ya malisho na mashamba vinavyoanza kuchipuka na kuibua hisia za sintofahamu.


Migogoro ya wakulima na wafugaji huanza kwa majibizano ya mara kwa mara kati ya wananchi wenyewe kwa kuingiliana katika maeneo yao jambo ambalo likipuuzwa ingali dogo hukomaa na kupelekea serikali kutumia nguvu nyingi katika kulimaliza.


Akizungumza na wakulima na wafugaji kwenye ziara ya kikazi katika vijiji korofi vinavyochagiza mgogoro huo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliwataka wananchi kuacha haraka kuibua hasira baina yao jambo ambalo linawezekana kutatulika.


Aliwataka wakulima ambao wamevamia katika maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya mpango wa matumizi bora ya ardhi kuondoka haraka katika maeneo hayo na kutafuta maeneo mengine kwa ajili ya kilimo kwani endapo kama watakiuka maelekezo hayo serikali itachukua hatua dhidi yao.


Aliwataka wakulima hao waliovamia maeneo hayo kufika ofisi ya Afisa Mtendaji wa kijiji ili kubaini kama wanastahili kupatiwa maeneo mengine kutokana na kukutwa katika maeneo hayo mara baada ya kuanzishwa sheria ya matumizi bora ya ardhi ya mwaka 2007.


Mhe Mtaturu alisema kuwa Mgogoro wa kimaeneo ya malisho na mashamba ambao umeanza kumea katika kipindi cha hivi karibuni Wilayani Manyoni unahusisha Vijiji jirani vya Itigi Mjini, Doroto na Damwelu vinavyochangia maeneo hayo.


Alisema kuwa ni lazima kila mwananchi kuwa wakala wa kuhifadhi na kutunza mazingira katika maneo yanayotuzunguka ikiwa ni pamoja na kutolima katika maeneo ambayo yamehifadhiwa au kupangwa kwa ajili ya mambo mengine.


Hata hivyo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi kufatilia ili kubaini aliyetoa maeneo ya wafugaji kwa wakulima ili achukuliwe hatua za kisheria kwani jambo hilo lina dalili zote za rushwa na uhujumu wa maeneo.


Sambamba na hayo pia Kaimu Mkuu huyo wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliwataka wananchi kuelekea msimu wa kulima mazao ya kipaumbele ambayo ni Pamba, Korosho, Chai, Kahawa na Tumbaku.


Aidha, alisema kuwa pamoja na mazao hayo ya kipaombele lakini wanapaswa kuongeza kasi katika kilimo cha mazao ya chakula na Biashara hususani mahindi, mtama, Dengu na zao la Alizeti.


Aidha, Mhe Mtaturu aliwashauri  wafugaji kupunguza idadi ya mifugo waliyonayo kwa kuuza na kununua au kujenga nyumba za kuishi ikiwa ni njia mojawapo ya kuweza kukidhi maeneo ya malisho yaliyopo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa