• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

MWENGE WAZINDUA NA KUWEKA MAWE YA MSINGI H'W ITIGI 2022

Posted on: August 14th, 2022

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Sahili Geraruma amewataka viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kusimamia ipasavyo miradi  mbalimbali ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati na kwa ubora unaolingana na thamani ya fedha ili iweze kuleta tija kwa jamii.

Geraruma amesema hayo wakati wa kuweka jiwe la Msingi katika mradi wa shule ya Sekondari Kitaraka iliyopo Halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni.

Amesema Wahandisi wanayo nafasi ya kushauri katika ujenzi kulingana na kiasi cha fedha zilizopo ili kujenga majengo machache yanayokamilika kwa muda mfupi na yakatumiwa na wanafunzi kuliko kujenga majengo mengi yasiyokamilika  kwa wakati uliyopangwa.

Ameongeza kuwa miradi mingi haikamiliki kwa wakati kwa sababu Wahandisi wanashindwa kushauri kulingana na taaluma zao jambo ambalo linachangia miradi hiyo kutokamilika kwa wakati na kujikuta inahitaji muda wa ziada.

Amewataka wasimamizi wa majengo hayo kuwa na Mpango kazi unaotekelezeka ili kujipima ufanisi na uwajibikaji wa kila mmoja.

Aidha akiwa katika kituo cha Afya Mitundu Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru ameagiza viongozi wasimamie misingi na maadili ya kazi zao huku akiwasihi mafundi kukagua vifaa vya ujenzi kabla ya kuvipeleka stoo.

Mmwenge wa uhuru ulikabidhiwa katika halmashauri ya Wilaya ya Itigi ukitokea wilaya ya Ikungi  mkoani Singida na kuweka jiwe la msingi mradi wa maji katika kijiji cha Gurungu wenye thamani ya shilingi 199,376,769.22,Uzinduzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya sekondari Kimadoi wenye thamani ya shilingi milioni 80, huku Jiwe la msingi likiwekwa katika kituo cha Afya Mitundu kilichojengwa kwa gharama ya shilini  milioni 251,310,000,sambamba na kutembelea mabanda ya Lishe,UKIMWI na Maralia katika kijiji cha Itagata pamoja na kuzingua klabu ya kupinga Rushwa katika shule ya sekondari ya Mitundu.

                                                                                                            Mwisho 

Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.