• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Itigi awataka Madiwani na Watumishi kufanya Kazi kwa ushirikiano kukidhi Mahitaji ya wananchi.

Posted on: December 16th, 2020

Na Luganuzi Muwelu.  H/W-ITIGI

Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Mh, Hussein Ibrahimu Simba Ambaye pia ni Diwani wa kata ya Tambukareli Amesema kuwa Waheshimiwa  Madiwani na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Itigi wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa

ili kukidhi na kutoa huduma bora kwa wananchi. Mh Simba amesema kuwa Wananchi hawa wanategemea huduma bora na hawahitaji migogoro kati ya Mh Diwani na Mtendaji

Aidha Mh.Simba Amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo  Bw  John K. Mgalula kwa kusimamamia ukusanyaji mzuri wa mapato ya ndani pamoja  Mweka hazina wa Halmashauri  Hiyo Bi Neema Lumambo kwa kuwa mipango mizuri ya ukusanyaji na ufuatiliaji mzuri wa Mapato hayo ambapo hapo Awali makusanyo ya ndani yalikuwa kidogo tofauti na sasa ambapo Makusanyo ni zaidi ya Million 100  kwa Mwezi.

Mh Simba pia amewataka Waheshimiwa Madiwani kwenda kusimamia upungufu wa Madawati Katika shule zao na Wanafunzi wote ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanakwenda shule na  kushirikiana na Watendaji kuchukua hatua kwa Wazazi watakaobainika kuwazuia watoto waliofaulu kutokwenda shule kwa namna moja ama nyingine.

Aidha Simba ametoa shukrani kwa Waheshimiwa madiwani wote kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo ya kuongoza halmashauri kwa nafasi ya uenyekiti wa halmashauri kwa miaka mitano na kuahidi ushirikiano mkubwa kati yake na Madiwani, Wananchi na Watendaji wote wa Serikali katika lengo moja tu la kuwatumikia wananchi na kuhakikisha huduma bora zinazotakiwa kutolewa zinatolewa.

Nae   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi  Bw. John K. Mgalula amesema kuwa yeye kama katibu wa baraza la Madiwani ataendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha shughuli zote za serikali zinafanyika kwa ukamilifu wake

Katika hatua Nyingine Mkuu wa Wilaya ya Manyoni na Mgeni Rasmi Bi Rahab Mwangisa amewataka Waheshimiwa Madiwani kuwa daraja kati ya Wananchi na Serikali na kuhakikisha changamoto ambazo zinawakabili wananchi zinatatuliwa kwa wakati .  

Aidha Mh Mkuu wa Wilaya Amewataka Madiwani kwenda kuhamasisha  wananchi ujiungaji wa mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa  ambayo itawasaidia wananchi hao kupata Matibabu kuanzia ngazi  Zahanati   mpaka Hospitali ya Mkoa kwa Kiasi cha Sh 30,000 tu kwa kila Kaya. Mwangisa Amesema  kuwa ni vizuri kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya  ili wananchi wahamisike kujiunga ambapo itawasidia katika suala zima la Matibabu pale mmoja wa familia anapoumwa

Awali uchaguzi wa ulifanyika wa kumchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi na Kupelekea Mhe Diwani wa Tambukareli Husseni Simba Kuibuka Mshindi Kwa kupata kura 18 za Ndio na Kura 1 ya hapana na kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya  Itigi na Makamu Mwenyekiti Mhe. Diwani wa Kata ya Mwamagembe  Jonathan Dulle Kuibuka Mshindi kwa kupata kura 16 za ndio na Kura 3 za hapana.

Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.