• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

NITASHUGHULIKIA MALALAMIKO YA AJIRA SGR-DC,MANYONI

Tarehe ya Kuwekwa: November 12th, 2022

Mkuu wa wilaya ya Manyoni  Bi.Rahabu Mwagisa amesema atafuatilia kwa makini utaratibu unaotumika kutoa ajira  katika mradi wa ujenzi wa reli ya treni ya mwendokasi kutoka na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.

Akizungumza na wakazi wa Mji wa Itigi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Songambele,kata ya Tambukareli Mkuu huyo wa Wilaya ya Manyoni amesema mradi wa SGR unatarajia kutoa nafasi za ajira takribani mia tano kwa Wilaya ya Manyoni na kwamba ajira hizo zitatolewa kwa awamu.

Baada ya kusikiliza kero na maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi waliofika katika mkutano huo  Mwagisa amesema kuwa amepokea meseji nyingi za malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya namna ajira hizo zinavyotolewa na kupelekea wananchi kukosa imani na mchakato mzima wa zoezi hilo.

Amebainisha kuwa utaratibu wa ajira ulivyo katika mradi huo ni kwamba wananchi katika maeneo yanayopitiwa na mradi wanapaswa kupewa kipaumbele lakini amekuwa akipokea malalamiko kuwa wanao ajiriwa ni wageni kutoka nje ya maeneo mradi ukakopitia.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema amesema atakutana uongozi wa Kampuni ya Yapi Markez  inayotekeleza mradi wa SGR ili kuzungumzia suala hilo .

‘’Nitakutana na Waturuki nifanye nao mkutano nadhani kuanzia wiki ijayo ili tuweze kubaini tatizo lilipo, kama ni wao au kuna watu wanatumika tuweze kudili nao’’alisema Mwagisa

Baadhi ya wananchi waliozungumzia suala hilo mbele ya Mkuu wa wilaya aliye ambatana na timu yake ya wataalamu kutoka Manyoni pamoja na halmashauri ya Itigi ni pamoja na Bwana Mayoi Elieza,Hamisi Samade na Yussuf Muhuta wamebainisha changamoto za mchakato wa upatikanaji wa ajira katika mradi wa SGR ni pamoja na umbali wa mahali/ kituo cha kufanyia usaili ambapo kwa sasa wanalazimika kwenda Tabora,pamoja na kuwepo kwa viashiria vya rushwa na kumuomba Mkuu wa wilaya kuwasaidia ili anayestahili kupata ajira  apate.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa