• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

SHAMBA LA SERIKALI LA KITARAKA KUFANYIWA UENDELEZWAJI

Tarehe ya Kuwekwa: July 8th, 2023

Shamba la serikali lililopo katika Halmashauri ya wilaya ya Itigi Mkoani Singida lipo katika mpango wa kufanyiwa uendelezaji na serikali ili kuleta tija kwa taifa  

Akizungumza na wananchi katika vijiji vya Kitaraka,Doroto na Kazikazi vinavyopakana na shamba hilo lenye ukubwa wa takribani ekari elfu 45  Mkurugenzi msaidizi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu na Mratibu wa Kamati ya Wataalamu ya kufanya utambuzi na tathmini ya shamba hilo Bi. Lina Kitosi amesema katika nyakati tofauti serikali imekua ikiangalia namna bora ya matumizi ya shamba hilo.

Amesema serikali ina nia thabiti ya kulifanyia uendelezaji shamba hilo hivyo Kamati inahitaji taarifa sahihi kuhusu idadi ya wananchi wanaolima katika shamba hilo ili serikali iweze kupanga matumizi kwa utaratibu unaofaa ili kuepuka mgogoro na kuwa na maslahi kwa pande zote mbili.

Naye Mbunge wa Jimbo la Manyoni magharibi Mhe. Yahaya Massare amewataka wananchi kutokuwa na hofu kwa kuwa serikali inataka kutambua eneo la shamba hilo na kuandaa mgawanyo kwa ajili ya matumizi ya serikali pamoja na wananchi huku akiimba Kamati hiyo kuchukua maoni ya wananchi ili kuepusha migogoro.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Itigi Mhe. Hussein Simba amewaomba wananchi kutoa ushiikiano kwa Kamati inayoratibu zoezi hilo na kukubali maelekezo kwa kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha shamba hilo linapangwa na  kutumika kwa njia inayofaa kwa maslahi ya taifa.

Baadhi ya  wakulima wanaolima katika shamba hilo Bw.Stephano Mwakijengi na Jackson Philipo wakaazi wa kijiji cha Kitaraka wameiomba serikali kufanya tathmini yakinifu ili kubaini maeneo ambayo yanaweza kutengwa kwa ajili ya matumizi ya wananchi kwa shughuli za kilimo na ufugaji.

Kamati hiyo maalumu imejumisha wajumbe kutoka ofisi ya Waziri Mkuu,ofisi ya Rais TAMISEMI,Wizara ya mifugo,Maliasili,Ardhi,Mambo ya ndani,Ujumbe kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Singida pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Itigi


Matangazo

  • TANGAZO LA KUKODI MAGARI KWA AJILI YA KAZI ZA MITIHIANI YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI , SEPTEMBA 12 HADI 14,2023 August 17, 2023
  • TANGAZO LA KAZI YA KATIBU MAHSUSI July 14, 2023
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WA AJIRA MPYA WALIMU NA KADA YA AFYA WALIOPANGIWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA ITIGI July 06, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATUNZA KUMBUKUMBU WALIO FAULU USAILI WA MAHOJIANO ULIO FANYIKA TAREHE 23/11/2022. December 09, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MHE.RIDHIWANI AZUNGUMZA NA WANUFAIKA WA TASF ITIGI DC

    August 28, 2023
  • DC.LWOTA AZINDUA ZAHANATI KITONGOJI CHA IKANAMALENGA

    August 24, 2023
  • WANANCHI KATA YA IPANDE WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MASUALA YA AFYA

    August 21, 2023
  • WALIMU WA SAYANSI ITIGI DC WAPIGWA MSASA

    August 12, 2023
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0737235630

    Simu ya Mkononi: 0757226612

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa