• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi watakiwa kuchangia Miradi ya Maendeleo-Minja

Posted on: October 12th, 2018

Kamati ya uchumi, uongozi na Mipango imewataka wananchi wa halmashauri ya Wilaya ya Itigi kuchangia Miradi ya maendeleo katika Maeneo yao. Kamati hiyo inayoongozwa na Mh Ally J Minja na Mwenyekiti wa Halamshauri ya Wilaya ya Itigi  Imewataka Wananchi hao pale ilipotembelea Miradi ya Maendeleo katika kata na vijiji Mbalimbali katika halmashuri ya Wilaya ya Itigi

Kamati hiyo ilifanya Ziara yake ya kukagua Miradi ya Maendeleo kwa kuanzia Kata ya Idondyandole kijiji cha Mbugani kwa kukagua na kujionea Mradi wa Ujenzi wa Zahanati ambao mradi huo unatokana na nguvu za Wananchi. Kata ya Aghondi kamati ilitembelea pia mradi wa Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Mabondeni ambapo kwenye mradi huu wananchi wameanza kwa Kujitolea kuchimba Msingi  kwa Ajili ya Kuanza ujenzi wa Zahanati hiyo  

Hata hivyo kamati iliendelea na ziara yake hiyo kwa siku ya kwanza katika kata ya Ipande katika kijiji cha Damwelu na kukagua na kujionea Ujenzi wa  shule Shikizi ya Mgamboo pamoja. Katika kata ya Tambukareli kamati ilitembelea katika Shule ya Msingi Mji mpya na kujionea Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa  na Ofisi 1 ya Walimu. Pia kata hiyo ya Tambukareli kamati ilitembelea shule shikizi kihanju. 

Kamati pia ilitembelea Mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Mitundu B na kuona ujenzi wa matundu 22 ya Vyoo katika kata hiyo ya Mitundu kamati pia ilitembelea Mradi wa maji wa pump ya Mkono 

Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ilimazia ziara yake katika Kata ya Kalangali kijiji cha Tulieni na kujionea ujenzi wa vyumba madarasa pamoja na ujenzi wa Zahanati 

Kamati ya uongozi na Mipango iliendelea na kutembelea Miradi siku pili kwa kutembelea Miradi katika kata ya kalangali ,Mwamagembe na kata ya Rungwa . katika kata ya Mwamagembe kamati ilimbelea ujenzi wa Shule shikizi itumba , Shule shikizi wila na Shule Shikizi Ngilimalole pamoja na kutembelea ukarabati wa kituo cha polisi mwamagembe  na kutembelea eneo ambalo kata ya Mwamagembe inapendekeza kujengwa kwa Shule Sekondari. Pia katika kata ya Rungwa kamati ilitembelea Ujenzi wa Bwawa la rungwa, Ukarabati wa Kituo cha Polisi Rungwa , Ujenzi wa Pump ya Mkono ya Maji pamoja na Ujenzi wa Daraja la Gwata

Kamati ya fedha uongozi na Mipango ikipokea Taarifa ya Ujenzi wa Pump ya Mkono katika Kata ya Mitundu halmashauri ya Wilaya ya Itigi

Mwenyekiti wa kamati ya fedha, uongozi na Mipango na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Itigi Mh Ally J Minja akimtwisha mwananchi ndoo ya maji

Ujenzi wa matundu ya vyoo ya katika shule ya Msingi Msingi Mitundu B

Kamati  ya fedha uongozi na Mipango ikipokea Taarifa ya Ujenzi wa Madarasa Shule ya Msingi Tulieni katika Kata ya Kalangali

Mwenyekiti wa kamati ya Fedha uongozi ,na mipango Mh Ally Minja Akizungumza na Wanafunzi katika shule ya Msingi Kalangali


Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.