• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

Wananchi wa Itigi waupokea Mwenge wa uhuru kwa shangwe

Posted on: August 9th, 2018

 

Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Itigi waupokea Mwenge wa uhuru kwa shangwe. Wananchi hao pamoja na Viongozi mbalimbali wameupokea Mwenge huo wa uhuru katika kata ya idodyandole katika kijiji cha kashangu ambapo Mwenge huo Ulipotokea katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni

Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Itigi akiupokea Mwenge huo kutoka kwa Charles Fussi Mkurugenzi wa Wilaya ya Manyoni alisema kuwa ameupokea mwenge huo na Utakimbizwa katika halmashauri ya Wilaya ya Itigi na kufanya kazi za Kuweka Mawe ya Msingi , kutembelea   na  Kuona Miradi Mbalimbali katika Halmashauri hiyo.

Baada ya Mapokezi hayo Mwenge wa Uhuru ulianza kukimbizwa kuelekea kijiji cha Ipangamasasi na kuweka jiwe la msingi  la ujenzi wa Vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja, Matundu 4 ya Vyoo vya wanafunzi pamoja na tundu moja la choo cha Walimu

Aidha katika hatua nyingine mkimbiza Mwenge kitaifa Mhandisi Charles Kabeho aliweza kutoa pongezi na kutoa cheti kwa  Mwanachi ambaye alitoa eneo hilo ili shule iyo iweze kujengwa pamoja na ivo kabeho aliweza kutoa shukrani zake za dhati kwa Walimu wawili ambao wamekuwa wakijitolea muda wote kuwafundisha wanafunzi hao  ambapo wanatoka umbali wa kilomita 13 kutoka shule mama ya Idodyandole

Kabeho pia aliweka jiwe la Msingi katika Zahanati ya Mbugani na kuwashukuru  sana  Wananchi kwa kutoa nguvu zao kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ambayo itawasaidia katika kupata matibabu. Katika hatua nyingine Mkimbiza mwenge wa Uhuru alikabidhi  vyandarua kwa wajawazito na kuwataka kuvitumia  vyandarua hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa

Pia mkimbiza mwenge aliweka jiwe la msingi katika Mradi wa maji unaotumia nishati ya Upepo katika kata ya Majengo kijiji cha Ziginali kwa niaba ya Mapepea 16  ambayo yamekarabatiwa 14 na 2 yametengenezwa upya.

Mkimbiza Mwenge Kitaifa Mhandisi Charles Kabeho Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kwa kuwa na Miradi mizuri na yenye tija kwa Wananchi

Katika Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Mkiwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ikungu  Mh Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwangisa alimshukuru mkimbiza mwenge kitaifa kwa kuukimbiza mwenge wa uhuru katika Wilaya ya Manyoni ambapo kuna Halmashauri mbili ya Manyoni na Halmashuri ya Wilaya ya Itigi na Kuweza kufungua , kuweka , kutembelea na kuona miradi mbalimbali ambayo itawasidia sana wananchi katika shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi n.k

Mh Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Itigi akiwa pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya wilaya Itigi katika eneo la mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha kashangu Kata ya Idodyandole

Wananchi  na Wataalamu wakiserebuka katika maandalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kijiji cha kashangu Kata ya idodyandole

Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.