• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

WANANCHI WAHIMIZWA KUTUNZA CHAKULA

Posted on: August 10th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota amewataka wananchi kutunza na kuweka akiba ya chakula ili kuepuka changamoto ya uhaba wa chakula katika kipindi cha msimu wa masika.

Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi pamoja na mambo mengine amewaagiza Madiwani kuwakumbusha wananchi katika maeneo yao kutunza chakula walicho nacho kwa kuwa taarifa za awali za hali ya hewa zinaonesha huenda kukawa na kiwango kikubwa cha mvua na kusababisha changamoto katika shughuli za kilimo.

Aidha Mhe Lwota ameiagiza Halmashauri kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato pamoja na kukamilisha ujenzi wa Maegesho ya maroli ili halmashauri iweze kukusanya mapato.

Wakati huo huo, Mhe Lwota amezitaka taasisi za TANESCO,TARURA na RUWASA kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa wakati pamoja na kuhudhuria vikao vya kikanuni katika halmashauri hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Itigi Mhe. Hussein Simba amewasisitiza Waheshiwa Madiwani na wataalamu katika Ofisi ya Mkurugenzi kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuwasaidia wananchi kufikia maendeleo .

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Manyoni Ndg.Jumanne Makanda ameipongeza Halmashauri ya Itigi kwa kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuendelea kutekeleza ilani inayobeba maono ya serikali huku akiiomba sekta ya maliasili kuwasaidia wananchi katika suala la ulinzi kutokana na uvamizi wa wanyama pori ikiwemo tembo ambao wamekuwa wakisababishia hasara wananchi.

Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.