• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

WATUMISHI WA UMMA WAKUMBUSHWA KUZINGATIA KANUNI ZA MAADILI YA UONGOZI

Posted on: September 7th, 2022

Watumishi wa umma wametakiwa kufanya  kazi kwa weledi na kwa kuzingatia kanuni ,sheria ,taratibu za maadili ya uongozi ili kuepuka migongano ya kimaslahi katika jamii na kusababisha watu kukosa  imani na taasisi za umma.

Hayo yamesemwa na Katibu msaidizi Idara ya Ukuzaji wa Maadili kutoka Ofisi ya Rais Sekritarieti ya Maadili ya Watumishi wa Umma Ndugu Salvatory Kilasara katika kikao kazi kwa watumishi wa Halmashauri ya Itigi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya  halmashauri hiyo.

Ndugu Kilasara  amesema kuwa  kuna baadhi ya mambo ambayo watumishi wa umma hawapaswi kufanya kulingana na miongozo ya kanuni za maadili ya utumishi wa umma ili kuepuka kuingia katika migongano ya kimaslahi ikiwa ni pamoja kupokea zawadi kutoka kwa wananchi.

Aidha Mkufunzi huyo amewakumbusha watumishi kuwa waaminifu na wakweli kwa  kuheshimu dhamana walizopewa huku wakizingatia  tamko la uadilifu walilolitoa  wakikumbuka kuwa wanawajibika mbele ya jamii na taifa.

Kwa upande wake Afisa Uchunguzi mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais Sekritarieti ya Maadili ya Watumishi wa Umma Bi.Modesta Anatoli Mtui amesisitiza watumishi kuwa  makini na matumizi taarifa  akisema kuwa siyo kila taarifa za kitaasisi ni taarifa za wazi huku akibainisha kuwa moja ya malengo ya viongozi wa umma ni kujenga imani kwa wananchi kwa serikali yao.

Bi.Mtui ameongeza kuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kila mtumishi atapimwa kulingana na uwajibikaji wake na kwamba atalazimika kuwajibika kibinafsi kulingana na  matkeo mabaya ya uwajibikaji wake.

Awali akifungua kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi Bwana John Mgalula ametawaka watumishi hao kuzingatia maelekezo watakayopata katika kikao kazi hicho kwa kuwa yatawasaidia kuboresha utendaji kazi wao wa kila siku.

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi Mh.Hussei Simba amewashukuru maafisa hao kutoka Ofisi ya Rais Sekritarieti ya Maadili ya Watumishi wa Umma kwa mafunzo hayo kwa kuwa yataleta tija kwa viongozi hao kwa wanachi na taifa kwa ujumla.

Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.