• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

Utaratibu wa Uhamisho kwa Watumishi

1 Mamlaka za Uhamisho

Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8. ya mwaka 2002 ikisomwa na Kanuni zake pamoja na Taratibu za Uendeshaji za mwaka 2003 Mamlaka ya Uhamisho kwa watumishi wote wa Umma ni Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na

Kwa maelekezo ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma kwa barua Kumb Na. C/CB.271/431/01/62 ya tarehe 8/06/2006 na Kumb Na. C/CB.271/431/01/J/144 ya tarehe 27/08/2007 Mamlaka ya Uhamisho katika Uhamisho wa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yamekasimiwa kwa;

  1. Katibu Mkuu Ofisi Ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa watumishi wanaohama kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine nje ya Mkoa;
  2. Katibu Tawala Mkoa kwa uhamisho wa watumshi wanaotoka Halmashauri moja kwenda nyingine ndani ya Mkoa na;
  3. Mkurugenzi wa Halmashauri kwa watumishi wanatoka kituo kimoja kwenda kingine ndani ya Halmashauri.

2. Aina za Uhamisho

Kuna aina mbili za Uhamisho, nazo ni;

  1. Uhamisho wa Kuomba
    1. Taratibu za Kuomba Nafasi:-

    2. Mtumishi atapaswa kuomba nafasi ya uhamisho kwa kuwasilisha maombi yake ya uhamisho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri au Mamlaka anayotaka kuhamia kupitia kwa Wasimamizi wake wa kazi katika kituo chake cha kazi alichopo na Mkurugenzi wake.
    3. Wasimamizi wa mtumishi anayeomba uhamisho watapaswa kuhakikisha maombi ya mtumishi yanafika katika mamlaka husika yakiwa na maoni yao kuhusu maombi hayo na sio kuzuia maombi. Iwapo kutakuwa na sababu ya msingi ya kuzuia maombi mwajiri amjulishe mtumishi kwa kumrejesha katika miongozo iliyopo
    4. Iwapo Mwombaji hataridhika na maoni /sababu za mwajiri /Msimamizi wa kazi kukataa maombi yake mwombaji atawasilisha maombi yake kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwa ushauri na kama hataridhia maombi yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yakiwa na vielelezo muhimu kuthibitisha maombi hayo kukataliwa na Mkurugenzi na kueleza sababu za yeye kuomba uhamisho huo.
    5. Mkurugenzi/Msimamizi wa kazi atayeombwa nafasi ya kuhamia atapaswa kumjibu mtumishi kupitia kwa Mkurugenzi wake kwa barua akimweleza kupatikana kwa nafasi hiyo kumetokana na nini ikiwa ni pamoja na kutaja Check Namba za watumshi waliofariki au kuacha kazi.
    6. Iwapo mtumishi wa umma ataomba uhamisho kwa sababu za kumfuata mume au mke, kujiandaa kustaafu baada ya kukaa miaka kumi nje ya mkoa anaotarajia kustaafia na kukaa katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitano anaweza kufikiriwa kugharamiwa gharama za uhamisho hata kama ataomba uhamisho mwenyewe.
    7. Mtumishi anayeomba uhamisho atapaswa kuwasilisha maombi yake kwa Katibu Mkuu au Katibu Tawala Mkoa au Mkurugenzi akiambatanisha barua iliyomkubalia kuhamia katika kituo anachotaka kuhamia. Aidha ni muhimu amjulishe mwombaji iwapo atagharimiwa uhamisho au la kufuatia kupata nafasi hiyo
    8. Upatikanaji wa Majibu:-

      Hairuhusiwi Mtumishi yeyote kutumia mtu mwingine isipokuwa yeye mwenyewe au Mwajiri wake kwa njia ya posta au Mkono kuwasilisha maombi yake ya uhamisho. Inashauriwa kutumia njia ya EMS au regista kwa urahisi wa ufuatiliaji.

      Angalizo:

    9. Watumshi wote walioomba uhamisho watapata majibu yao kwa barua kupitia kwa waajiri wao na sio vinginevyo.
    10. Aidha kwakuwa uhamisho huu ni wa wazi watumishi waliokubaliwa au kaukataliwa uhamisho watapata taarifa za awali kupitia Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yaani www.pmoral.go.tz mapema mwezi Julai kwa maombi yatakayopokelewa kuanzia Januari hadi Juni na mapema mwezi Januari kwa maombi yatayopokelewa kuanzia mwezi Julai hadi Desemba kwa kuwa Ofisi yetu imejipanga kushughulikia masuala ya uhamisho mara mbili kwa mwaka ili kuepusha mwingiliano wa majukumu katika vituo vya kazi kwa mwaka.
    11. Mtumishi atakayekuwa na malalamiko kuhusu maombi yake ya uhamisho anashauriwa kuelekeza maombi yake kwa Mamlaka iliyomwamisha kupitia kwa mwajiri wake na msimamizi wa kazi akiambatisha maombi yake ya awali na vilelezo vingine muhimu kama sababu za kuomba uhamisho na ushahidi wa kufikisha barua yake kwa Mamlaka ya uhamisho.
    12. Malalamiko ya mtumishi aliyeomba uhamisho na hakupata majibu au hakuridhika na majibu aliyopatiwa malalamiko yake yatashughulikiwa ndani ya siku saba bila kujali muda wa uhamisho yaani June au Desemba.
    13. Baada ya mtumshi kupata majibu /barua ya uhamisho atapaswa kuripoti ndani ya siku kumi na nne tangu amekabidhiwa barua yake ya uhamisho vinginevyo atachulikuliwa ni mtoro kazini

kwa maelezo zaidi tembelea http://www.tamisemi.go.tz/information-left/habari-1002-20150219-Utaratibu-wa-Uhamisho/

Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.