• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

Baraza la Madiwani Itigi laishukuru serikali kwa kupata fedha za Miradi ya Maendeleo

Tarehe ya Kuwekwa: April 30th, 2021

Na Luganuzi Muwelu -Itigi dc

Baraza la Madiawani Itigi limeishukuru Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa Miradi Mbalimbali inayoendelea katika Maeneo mbalimbali katika kata tofauti tofauti katika halmashauri ya wilaya ya Itigi

Mh Mwenyekiti  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Itigi  Hussein Simba ameyasema hayo kwenye kwenye kikao cha baraza la Madiwani  kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Itigi baada ya Mkurugenzi Mtendaji Kuwasilisha Kiasi cha Fedha za miradi  kilichongia  katika utekelezaji na ukamilishaji wa miradi mbalimbali katika halmashauri ya Itigi

Simba amesema kuwa “ tunaishukuru serikali kwa kutuletea fedha za ujenzi wa miradi mbalimbali
ikiwemo mradi wa ujenzi wa mabweni ya wasichana mawili katika shule za sekondari ya Ipamuda na Mgandu, ujenzi wa Matundu ya vyoo katika zahanati, ujenzi wa nyumba za watumishi na miradi mingineyo”

Aidha simba amesema kuwa “sisi madiwani tushirikiane na wananchi katika maeneo yetu  tuhakikishe miradi tulioletewa na serikali inakamilika kwa wakati”

Akitoa taarifa hiyo Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Itigi Bi Grace N. Mwaigaga amesema kuwa” Halmashauri ya Wilaya ya Itigi tumepokea fedha za miradi mbalimbali ikiwemo fedha za ujenzi wa matundu ya vyoo katika zahanati kiasi cha Tsh 66,000,000/= Fedha za ujenzi wa Maabara  katika shule  za sekondari kiasi cha Tsh 130,000,000/= fedha za ujenzi wa Nyumba za watumishi kiasi cha Tsh 470,000,000 Fedha kwa Ajili ya Matundu ya vyoo kiasi cha Tsh  13,000,000/= Shule ya Sekondari Itigi sekondari  Pamoja na fedha za ununuzi wa Magari 3 kiasi cha Tsh 220,000,000/=

Aidha Bi Mwaigaiga amesema kuwa Halmashauri ya wilaya ya itigi itahakikisha Miradi yote kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika watahakikisha fedha zote zitafanya kazi kama ilivyokusudiwa na Miradi yoye itakamilika kwa wakati

Katika hatua nyingine Meneja wa Tarura halmashauri ya Wilaya ya Itigi ambae alikuwa ni Mgeni Mkaribishwa kwenye Baraza hilo Mhandisi Daniel Mwiru amesema kuwa kwa sasa wapo katika utekelezaji wa barabara yenye urefu  Km 892 zilizopo katika kata na vijiji mbalimbali katika halmashauri ya Itigi 

Pamoja na kuendelea kufanya matengenezo ya barabara hizo tutaenendelea kutengeneza barabara nyingi kadiri tutakapo pata fedha

Naye Diwani  kata ya Rungwa Mh Saidi Yahaya Sudi  amewashauri Tarura kutengeneza barabara zenye ubora ambazo zinaweza kukaa kwa Muda mrefu bila kuharibika kuliko hivi sasa barabara ambapo barabara zikitenezwa zinachuka mda mfupi na kuharibika

Katika hatua nyingine baraza la madiwani hilo limewathibitisha kazini watumishi 7 , kuwapandisha Madaraja watumishi 64, kupitisha majina ya watumishi h odari 34 na kuwabadilisha Miundo ya Utumishi watumishi  21.

Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Bi Grace N. Mwaigaga (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi wa maswala mbalimbali katika baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Itigi

Mh Saidi Yahaya Sudi akichangia Suala la ujenzi wa bararaba kutoka Mkiwa -Rungwa (Aliyesimama) katika Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

 Mh  Diwani wa Viti Maalum Utukufu Gwimile (Aliyesimama)  akitoa Mchango wake katika Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

 Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili Ndugu John F. Makota (Aliyesimama) Akitoa Ufafanuzi wa Masuala mbalimbali ya Migogoro ya Ardhi katika Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa