• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

DC.LWOTA AZINDUA ZAHANATI KITONGOJI CHA IKANAMALENGA

Tarehe ya Kuwekwa: August 24th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kerembe Lwota amezindua Zahanati ya kata ya Ipande ambapo amesema ameridhishwa na jitihada za wananchi katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi huo iliyojengwa kwa nguvu za wananchi  pamoja na  fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri hadi kukamilika .

Akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Ikanamalenga katika uzinduzi huo, DC.Lwota amesema amewapongeza wananchi hao kwa juhudi zao katika shughuli za maendeleo hususani ushiriki wa wananchi katika ujenzi wa zahanati hiyo

Amesema kutokana juhudi na utayari wa wananchi serikali inayoongozwa na Mhe,Dkt Samia Suluhu Hassani,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa shilingi milioni hamsini(Mil.50) ili kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika na huduma za kiafya zinaanza kutolewa.

“Nimeambiwa kuna maeneo walianza mradi miaka mitatu nyuma na haijakamilika lakini hapa mmefaulu licha ya changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa maji, nawapongeza sana ”alisema, DC Lwota

 Aidha DC ametoa rai kwa wananchi kutunza mradi huo muhimu pamoja na kuwapa ushirikianao watumishi waliopangiwa kutoa  huduma za afya  katika zahanati hiyo ili waweze kutoa huduma stahiki kwa jamii.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Dkt.Emmanuel Mallange kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri amesema Wananchi walionesha jitihada kubwa kwa kujitolea kujenga  zahanati hiyo kufikia hatua ya lenta ndipo serikali kupitia mapato ya ndani ya halmashauri ikatoa kiasi cha shilingi milioni hamsini (Tshs 50,000 000/= ) ili kukamilsha mradi huo.

 Naye, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Manyoni Ndg. Jumanne Ismail Makanda amewataka wakazi wa Kata ya Ipande hususani akina mama kuitumia vizuri zahanati hiyo kwa kwenda kupata huduma kwa wakati.

“ Itakua ajabu kuona akina mama wajawazito wanajifungulia nyumbani na kujiweka katika hatari zinazotokana na changamoto za uzazi wakati serikali imewasogezea huduma katika maeneo yao “alisisitiza

Pia Diwani wa Kata ya Ipande  Mhe. Kedmond Mpondo amebainisha kuwa wazo la ujenzi wa zahanati lilitokana na mkutano wa wananchi walipokubaliana kujenga zahanati kama  kipaumbele kati ya mahitaji waliyo nayo.

“Mwaka jana [2022]  tulifanya kikao na wananchi na tukakubaliana kuwa tujenge zahanati kwa kujitolea nguvu zetu na ndipo serikali ikatuunga mkono katika hatua ya ukamilishaji”alifafanua  Mhe Mpondo

Mhe.Mpondo amewapongeza wananchi kwa kushiriki ipasavyo katika mradi huo licha Kitongoji hicho kuwa na changamoto kubwa ya uptikanaji wa maji .

Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya alitembelea Shule Shikizi ya Katumba,Zahanati ya Mkajenga pamoja na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi katika kitongoji cha Mkajenga.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa