• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

KAMATI YA SIASA MKOA WA SINGIDA YATEMBELEA MIRADI YA MAJI GURUNGU,KITARAKA.

Tarehe ya Kuwekwa: March 17th, 2022

   

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilis Mahenge amewataka wakazi wa vijiji vya Gurungu  na Kitaraja kutunza na kuulinda miradi ya maji inaojengwa katika vijiji vyao ili viweze kuwanufaisha kwa muda mrefu.

Dkt. Mahenge akiambatana na Kamati ya siasa yaMkoa amesema hayo leo alipotembelea ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji vya Gurungu Kata ya Sanjaranda na kijiji cha Kitaraka katika  Halmashauri ya Itigi na kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Aidha Dkt. Mahenge amempongeza Mhesimiwa Rais, Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika mkoa huu na nchi nzima kwa ujumla.

Awali akitoa taarifa za miradi Meneja wa RUWASA  wilaya ya Manyoni Eng. Gabriel Ngongi amesema kuwa mradi wa Kijiji cha Kitaraka umetengewa jumla ya shilingi milioni 200,fedha kutoka serikali kuu utawanufaisha watu zaidi ya elfu tatu(3085) katika kijiji hicho wakati fedha zaidi ya shilingi milioni miatatu sabini na tatu(Tsh,mil 373,8330,362)kutoka Serikali kuu zilitengwa kwa ajili ya mradi wa Kitaraka ambao utanufaisha watu zaidi ya elfu nne(4344).

Amebainisha kuwa mradi wa kijiji cha Gurungu uliibuliwa mwaka 2020 na kuingizwa katika bajeti ya serikali ya mwaka 2020-2021 na kuanza utekelezaji wake machi 7,2022 na unatarajiwa kukamilika mwezi mei mwaka huu, huku mradi wa maji wa kata ya Kitaraka uliibuliwa mwaka 2018 na kuingizwa katika bajeti ya serikali ya mwaka 2019-2020 na kuanza kutekelezwa Mei 2020 na kukamilika Aprili 30,2021.

Amesema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutapunguza kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kutumia muda mrefu kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za kiuchumi,wanafunzi kupata muda wa kutosha wa kusoma na kujiandaa sambamba kuondoa malalamiko ya wananchi  kwa viongozi wao.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA mkoa ,Eng. Lucas Saidi amesema kuwa tayari RUWASA imeshachimba kisima cha maji chenye ujazo wa lita elfu kumi na nne(14,000) kiwango kinachotosheleza mahitaji ya wakazi wa kijiji cha Kitaraka na maeneo ya jirani wakati kisima cha Kitaraka kinauwezo wa kuzalisha lita 5000 kwa saa.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi Mhe.Hussein Simba amesema kuwa asilimia sitini ya vijiji katika halmashauri yake vinapata maji safi na salama kutokana na miradi ya maji iliyotekelezwa na kuongeza kuwa anaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuipa kipaumbele halmashauri ya Itigi katika ujenzi wa miradi mbalimbali.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa