• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

KAMPENI"ONJAMA" KUIOKOA MANYONI NA BAA LA NJAA

Tarehe ya Kuwekwa: April 8th, 2023

Halmashauri ya  Wilaya ya Manyoni imekuja na mpango wa  kutokomeza baa la  njaa katika Wilaya hiyo kwa  kuibua Kampeni ya Ondoa  Njaa Manyoni (ONJAMA) kwa kuhamasisha wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame  kulingana na jografia ya eneo hilo.

Akizungumza katika Kikao cha Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Itigi Mkuu wa Wilaya ya Manyon Mhe.Kemilembe Lwota amesema  serikali imekuwa ikifanya kazi nzuri ya kuwapatia wananchi chakula cha bei nafuu katika maeneo yenye njaa ikiwemo wilaya ya Manyoni lakini amesisitiza kuwa utaratibu huo wa kutegemea serikali kuwapatia chakula ufike kikomo.

Amesema  pamoja na jografia ya Wilaya hiyo kuwa na mvua zisizotabirika  bado wananchi wanaweza kulima mazao ya chakula kama mihogo,mtama,uwele na mazao mengine ambayo yanaweza kuhimili mvua chache huku akiwataka madiwani kwenda kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kulima mazao ya aina hiyo ili kuepuka  baa la njaa kujirudia katika wilaya hiyo.

Kwa upande mwingine DC.Lwota amewataka Madiwani, Divisheni ya Elimu na viongozi wa ngazi ya Kata kuhakikisha wanafunzi wote wanaotakiwa kuwa shuleni katika hatua ya elimu msingi na sekondari kuripoti shuleni mara tu shule zitakapofunguliwa.

Amesisitiza kuwa serikali imefanaya kazi kubwa ya kujenga miundombinu bora ya elimu ikiwemo vyumba bora na vya kutosha vya madarasa lakini changamoto imebaki katika zoezi la uandikishaji wa wanafunzi na kusema kuwa jambo hilo halikubaliki.

Awali akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi Mhe. Hussein Simba amebainisha kuwa halmashauri hiyo kwa kiwango kikubwa inategemea makusanyo yanayotokana na mazao ya kilimo ambapo kufikia sasa makusanyo ya halmashauri ni takribani milioni 894 ikiwa ni sawa na  asilimia 47.

Mhe.Simba amebainisha mikakati ya kuongeza nyanzo vingine vya mapato ikiwa ni pamoja na kujenga maegesho ya maroli na stendi ya magari katika mji wa Itigi na stendi ya magari katika  kata ya Rungwa ambayo ujenzi wake unaendelea  kufikia sasa kwa gharama ya shilingi milioni thelathini huku akishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais,Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutekeleza miradi mikubwa  ya kimkakati Ili kutoa huduma kwa wananchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa