• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

MAFUNZO KAMPENI YA CHANJO YA POLIO HALMASHAURI YA ITIGI YAFANYIKA

Posted on: April 24th, 2022

Jamii imetakiwa kushiriki katika kampeni ya kitaifa ya chanjo ya ugonjwa wa polio awamu ya pili ili kuwakinga watoto wenye umri chini ya miaka mitano dhidi ya ugonjwa huo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wahamasishaji ngazi ya jamii kuhusu kampeni ya chanjo ya polio katika halmashauri ya Itigi Mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dk.victorine Ludovick amesema kampeni hii imekuja mara baada ya ugonjwa huo kuripotiwa katika nchi jirani ya malawi na kuongeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa ugonjwa huo kuingia nchini.

Dk.Ludovick amesema anaimani zoezi la utoaji chanjo ya polio katika halmashauri  ya Itigi litafanikiwa kwa asilimia mia moja kutokana muitikio mkubwa wa wahamasishaji ngazi ya jamii''naamini mtaenda kuwahamasisha watu washiriki kikamilifu zoezi hili muhimu ili tuweze kulikinga taifa letu dhidi ya ugonjwa huo hatari'' alisema Ludovick.

Naye muuguzi mkuu wa Mkoa wa Singida Bi,Hyasinta Alute amesema kuwa kwa sasa nchi ipo katika dharura ya kupambana na ugonjwa wa polio na kuwataka wadau  wa  afya watakaoshiriki katika zoezi hilo kuhakikisha kila mtoto anapatiwa chanjo.

 Mganga mkuu wa halmashauri ya Itigi Dk.Emmanuel Mallange akawapongeza wahamasishaji ngazi ya jamii kwa kuitikia wito wa dharura na kuhudhuria mafunzo hayo''mmechukua hatua ya kizalendo kuitikia wito wa dharura kuja kwenye mafunzo haya ya jinsi ya kutoa chanjo ya polio ikiwa ni kampeni ya kitaifa''amesema Dk Mallange.

Aidha Mwenyekiti wa kijiji cha Ipande na mhamasishaji ngazi ya jamii Bwana Julius Labia amesema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kuwa na uelewa wa kutosha juu ya ugojwa wa polio na pamoja na njia nzuri ya kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika kampeni hiyo.

Kwa upande wake Bi,Merry Amasi ambaye ni mhudumu wa afya ngazi ya jamii amewaomba wakazi wa halmashauri ya Itigi kuunga mkono zoezi hilo''watu wasiwe na hofu,wajitokeze kuunga mkono zoezi hili ili kuwakinga watoto wetu dhidi ya ugonjwa wa polio''.

Kampeni hii ya kitaifa ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio katika halmashauri ya Itigi itaanza tarehe 28 hadi 31 aprili kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano.



Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.