• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

MASUALA YA AFYA NA LISHE KUWA AJENDA YA KUDUMU HALMASHAURI YA ITIGI

Tarehe ya Kuwekwa: February 2nd, 2022


Idara ya Afya  ya Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kitengo cha lishe kimefanya kampeni ya vitamini A, Ugawaji wa dawa za kutibu minyoo tumbo na kufanya tathimini ya LISHE kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi sita hadi miezi hamsini na tisa (miezi 6 -59) ambapo walengwa wamefikiwa kwa asilimia 129.6 sawa na watoto 28372 kati ya walengwa 21881.

 Mratibu wa lishe na Muuguzi Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi,Bw. FREDERICK GAISHA amesema hayo wakati akiwasilisha TAARIFA YA UTEKELEZAJI MASUALA YA LISHE kwa kipindi cha robo ya pili ya  Oktoba hadi Disemba 2021 na kuongeza kuwa Halmashauri ilipanga kufanya jumla ya shughuli nane za afua za lishe kwa thamani ya shilingi12,091,000,hata hivyo Idara imefanikiwa kufanya jumla ya afua za lishe tatu kwa thamani ya shilingi 5,287,000.00 sawa na asilimia 43.7.

Aidha katika kipindi hiki cha robo ya pili  mkazo wa utoaji chakula / uji umeendelea kutolewa  katika shule ya Msingi Mlowa kwa wanafunzi wa Elimu maalum ikiwa jumla ya Shilingi 1,806,000 zikitolewa kutoka ruzuku ya serikali kuu huku  shule ya msingi Itigi –Reli,St. Vicent,St.Francis Exavier Maranatha nazo zikitekeleza mpango huo.

Bw. FREDERICK GAISHA amesisitiza kuwa viongozi wa Halmashauri kuanzia ngazi ya jamii, kisiasa ,kidini na wadau wote wa Afya washiriki katika kuhamasisha jamii kula MLO KAMILI kutoka makundi matano ya chakula na mtindo bora wa maisha  sanjari na akina mama kuanza  mapema kliniki ya ujauzito ili waweze kupata msaada wa kitaalam kwa wakati .

Akitoa maelekezo kwa Idara ya Afya MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO MH.JOHN MGALULA amesema pamoja na idara hiyo kufanya vizuri katika  afua za lishe lakini bado inahitaji kuongeza nguvu ili kuhakikisha  matatizo ya utapiamlo na udumavu pamoja na changamoto nyingine za kisekta zinatatuliwa kwa asilimia mia moja.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa