• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

MGANGA MKUU ITIGI DR MALLANGE AENDELEZA OPERATION FUNGIA MAABARA BUBU

Tarehe ya Kuwekwa: February 4th, 2020

Dr Emmanuel mallange ambaye ni mganga mkuu katika halmashauri ya Wilaya ya Itigi ameendelea na operation   ya kufungia maabara bubu ambazo zinatoa huduma za upimaji wa magonjwa katika kata na vijiji mbalimbali katika halmashauri ya itigi

Dr mallange akiwa na Timu ya ukaguzi   walifika katika kata ya ipande  katika  halmashauri ya wilaya ya Itigi wakiwa katika ukaguzi wa kawaida na kupata habari  kwa wananchi kuwa kuna Maabara ipo katika kata ya ipande kitongoji cha mngalalee  ambayo inatoa huduma za upimaji pamoja na huduma za uzalishaji ambapo inasadikika akina mama wawili wamejifungulia katika maabara hiyo bubu nyakati za usiku.

Baada ya kupata habari hiyo Dr Mallange na Timu yake walifika katika maabara hiyo na kukuta baadhi ya wagonjwa wakiwa wanasubiri kupata huduma za vipimo pamoja na kuandikiwa dawa ili wakanunue kwenye duka bubu ambalo halina usajili lililopo pembezoni mwa Maabara hiyo isiyokuwa na jina.

Muhudumu wa maabara hiyo bubu ambaye alifahamika kwa jina Moja la bwana Gasper alifanikiwa kukimbia baada ya kuona maafisa wa ukaguzi wanafika katika maabara hiyo. Hata hivyo Dr Mallange aliwachukua wagonjwa wote waliokuwa wanasubiri huduma katika maabara hiyo na kuwapeleka katika zahanati ya Ipande na kupatiwa matibabu ipasavyo. Pamoja na Mhuhudumu huyo kukimbia Dr Mallange amemtaka mmiliki wa nyumba hizo zinazoendelesha Maabara na Duka bubu bwana Robart Chalamaganza kufika Ofisini kwake haraka iwezakanavyo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha   Dr Mallange alitumia fursa hiyo kuwaelimisha wananchi na wagonjwa hao umuhimu wa kujiunga na Mfumo wa bima ya Afya ya jamii iliyoboreshwa ambapo wanachi hao waliona unafuu ni mkubwa sana kwao kwa kuwa na bima ambayo wanaweza kutibiwa kuanzia ngazi ya zahanati mpaka hospitali ya Mkoa na kuomba Afisa Muandikishaji awatembelee katika kaya zao ili waweze kuijunga na Mfuko huo ambao una faida kubwa sana katika kupata matibabu yenye unafuu.

Hata hivyo dr Mallange amewashukuru wananchi kwa kutoa taarifa za kutoridhishwa na utoaji huduma wa maabara na maduka bubu ambayo yanafanya kazi katika kata hiyo ya ipande

Aidha Timu hiyo ya ukaguzi imefungia maduka ya madawa   mawili bubu ambayo yanamilikiwa na bwana Robert Chalamaganza  pamoja na bwana Hamisi Abasi pamoja na kuchukua dawa zote pamoja na vifaa vyote vilivyokuwemo  katika maabara bubu. Kwa upande wake Mratibu wa Maabara wilaya Bi Pendo Kiula amesema kuwa uamuzi wa uchukuaji wa vifaa hivyo vya maabara unatokana na Maabara hiyo bubu kutokidhi hata kitu kimoja kati ya vigezo vinavyotakiwa katika ufunguaji wa maabara  ikiwemo Jina la maabara ,Aina ya Maabara ,Kibali /kuandikishwa ,Wafanyakazi wenye sifa ,Majengo/jengo n.k

Naye Petro Loya(39) mkazi wa kata ya ipande kitongoji cha msumbiji ambaye alikuwa na mgonjwa wake Jonas Julius (14) wameishukuru sana serikali kwa kufuatilia maabara hizo ambazo wakati mwingine wanakwenda kwa kupotoshwa kuwa Hospitali za serikali hazina dawa. Bwana Loya amesema kuwa mgonjwa wake baada ya kumpeleka zahanati ya ipande  amepata huduma nzuri za vipimo pamoja na kupewa dawa ambazo hakutegemea kama angeweza kuzipata.

Aidha bwana loya ameishukuru sana serikali kwa uanzishwaji wa mfuko wa bima ya Afya ya jamii kwa kuwa imemfanya mgonjwa wake atibiwe kwa gharama ndogo sana kuliko ambako angetoa fedha hizo kwenye maabara bubu ambako huwa anatumia kiasi cha sh 40,000 mpaka sh 30,000 kila wakati anapokwenda kwenye maaabara hizo. Pamoja na hivyo bwana  Loya amewaomba wanachi ambao hawajajiunga na Mfuko wa bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa wajiunge sasa kwa kuwa Ndio Mkombozi wao kwa kupata Huduma bora za Matibabu.

Jengo la Maabara Bubu inayotumika katika kijiji cha ipande lenye Mlango wenye geti jekundu na kiti cha kukalia wagonjwa (kushoto)Pamoja na Mlango wenye geti jekundu na Kiti cha kukalia wateja (kulia ) ambapo duka la madawa bubu ndipo ninapofanyia kazi

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Itigi Dr Emanuel Mallange (Kushoto) akiwa na Wagonjwa ambao wanasuburi kupata huduma  kwa kificho katika Nyumba ya bwana Robert Chalamaganza baada ya kuona timu ya Ukaguzi imefika katika Eneo hilo.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Itigi Dr Emanuel Mallange (katikati) Akitoa Msaada wa Kupakia wagonjwa ambao walikuwa hawajiwezi kwenye gari na Kupelekwa katika Zahanati ya Ipande kwa matibabu zaidi

Mratibu wa Maabara wilaya Bi Pendo Kiula(Kulia ) Pamoja na Mganga Mkuu (Kushoto) wakiangalia vifaa vilivyokutwa kwenye maabara Bubu iliyopo katika Kijiji cha Ipande katika Halmashauri ya Itigi

 Mganga Mkuu Dr Mallange Akiwafuatilia Wagonjwa kwa Usafiri wa Baiskeli wagonjwa baada ya Wagonjwa Hao kupelekwa katika Zahanati ya Ipande.

Mganga Mkuu Dr Mallange (kushoto) akiwa na bwana Petro Loya ambae amehamasishwa Umuhimu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii iliyobreshwa na kupelekea kujiunga na siku hiyo hiyo kwa sh 30000 .

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa