• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

Mganga Mkuu Itigi Dr. Mallange azifungia Maabara mbili kwa kukiuka utaratibu

Tarehe ya Kuwekwa: November 12th, 2019

Na Luganuzi Muwelu.

Mganga  Mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Itigi Dr Emmanuel Mallange amezifungia Maabara Mbili kwa kukiuka utaratibu wa Utoaji huduma za Maabara. Hatua hiyo ya ufungiaji wa maabara hizo mbili ambazo ni  Maabara inayojulikana New Harizon health Maabara Maarufu kwa Mkenya na Maabara inayojulikana kwa Jina la Mengi Maabara Maarufu kwa Dr Mengi ambapo Timu ya ukaguzi ya Wilaya ilipopita na kufanya Ukaguzi wa Maelekezo Mbalilmbali waliyoyatoa katika Robo ukaguzi Iliyopita na kuona Maabara hizo kutozingatia taratibu za utaoji wa huduma zikiwemo usafi pamoja kutoa vipimo ambavyo hawatakiwi kuvitoa

Mganga Mkuu dr mallange Akiwa na Timu ya Ukaguzi amewataka wamiliki wa Maabara hizo na Nyinginezo zinazotoa huduma katika halmashauri ya Itigi kutoa huduma kwa Kufuata taratibu zote za utoaji wa huduma Dr Mallange amesema kuwa hayuko tayari kuona maabara zinaenda kinyume na utaratibu. Serikali haitakubaliana na Wamiliki wanaotoa huduma kinyume na miongozo. Dr Mallange amesema pia  pamoja na Kuanza kuzifungia Maabara Hizi tutafuata sheria pamoja na kuwapeleka katika Vyombo vya Kisheria ili sheria ifuate mkondo Wake

Aidha Dr. Mallange Amewaeleza wagonjwa waliokutwa kwenye Maabara hizo zilizofungiwa kuwa  Kwa Sasa Halamshauri ya Wilaya ya Itigi katika Zahanati zake , Vituo  vya Afya kuna Dawa Za kutosha , huduma bora zinatolewa na Wauguzi waliopo hata Vipimo mmnavyovifuata  katika Maabara hizo Zahanati na Vituo vya Afya vinatolewa tena kwa Utaratibu Mzuri ni Vema wakati wote unapojisikia kuumwa uende kwenye zahanati au vituo vya Afya ili uonane na Wataalam

Dr Mallange amewaeleza pia Wananchi hao serikali kwa Sasa Imeanzisha Mfuko wa Bima ya Afya Iliyoboreshwa ambapo mwananchama wa Mfuko huo wa Bima Atapatiwa Matibabu kwa Gharama nafuu ya Sh 30000 tu yeye na Kaya  yake ya Watu 6. Ambapo Mwanachama anaweza kupata matibabu katika zahanati , vituo vya Afya na Hospitali katika ngazi ya Mkoa kwa Muda wa Mwaka 1

Naye Mratibu wa Maabara wilaya Bi Pendo Kiula amezitaka mabaara hizo kuzingatia Usafi katika maabara Hizo, Kutokutoa huduma ambazo Maabara hazistaili kama vile kuwa na Kipimo cha Kupimia Virusi vya Ukimwi, Kutokula Chakula Katika Maeneo ya Maabara , Kuwa na Vichomea taka vinavyokidhi vigezo

Bi mbuke Maige (57) Mkazi wa kitaraka katika halmashauri ya Itigi alikutwa na timu ya Ukaguzi akiwa ameenda  kuchoma sindano ambazo alianzishiwa na maabara Hiyo ya New Harizon Health . Bi mbuke  aliyeambatana na Mkwe wake Rabeka Mboje (20) walisema kuwa waliandikiwa dawa pamoja na kuambiwa wahudhurie sindano kila siku saa 11 jioni na kila wanapofika wanatoa kiasi cha fedha sh 20000 kwa ajili ya sindano

 Bi mbuke alimshukuru mganga mkuu kwa kufanya Operation hiyo ambayo kimsingi itawaokoa wananchi wengi ambao wanatapeliwa na matapeli ambao wanajidai ni wataalamu wa Afya na kutoa huduma zisizofuata utaratibu

Maabara inayojulikana kwa jina la New Harizon health Labaratory maarufu kwa Mkenya iliyofungiwa na Timu ya ukaguzi

Maabara inayojulikana kwa jina la New Harizon health Labaratory maarufu kwa Mkenya iliyofungiwa na Timu ya ukaguzi

Maabara inayojulikana kwa jina la Mengi Maabara maarufu kwa Dr Mengi iliyofungiwa na Timu ya ukaguzi

Wagonjwa waliokutwa katika maabara hizo wakisubiri kuchomwa Sindano

Mganga mkuu Dr mallange (kulia) Akifurahia jambo na mgonjwa Aliyemtoa na Kumpeleka katika kituo cha Afya itigi na kupatiwa Matibabu

 Mratibu wa maabara wilaya akielezea taratibu za uendeshaji wa Maabara.


Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa