• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

MPANGO WA BAJETI 2022-2023 WAAKISI MAENDELEO HALMASHAURI YA ITIGI

Tarehe ya Kuwekwa: January 28th, 2022


Halmashauri ya Wilaya ya Itigi ilikisia kupokea Ruzuku na kukusanya mapato ya ndani zaidi ya bilioni kumi na tano(15,231,229,907.00)kwa mwaka wa fedha 2020-2021.

Akiwasilisha taarifa ya mapitio ya mwaka 2020-2021, mwenendo wa bajeti ya mwaka 2021-2022 na mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Bw.Regan Daniel Mumba  amebainisha vyanzo mbalimbali  ambavyo Halmashauri  imekusanya mapato ikiwa ni pamoja na mapato ya ndani,ruzuku kutoka serikali kuu na wadau wa maendeleo.

Aidha Halmashauri iliidhinishiwa kutumia kiasi cha Tsh.15,265,635,270.00 kwa matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mishahara,matumizi ya mengineyo na miradi ya maendeleo.

Akichangia hoja kuhusu randama ya mapendekezo ya Mpango wa Bajeti hiyo Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh. Rahabu Mwagisa  ameipongeza halmashauri ya Itigi kwa mwenendo wake wa ukusanyaji mapato na matumizi hasa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya  amesema kuwa pamoja na halmashauri hiyo kutekeleza  kwa wakati na kwa viwango miradi ya ujenzi wa madarasa amesema kuwa mahudhurio ya wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu ni kwa kiwango chini na kuitaka halmashauri hiyo kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa wanaripoti shuleni.

Akizungumzia hali ya kilimo ,Mkuu wa Wilaya ameiagiza halmashauri kuhakikisha mbegu za alizeti  aina ya Record zilizoletwa na serikali zinawafikia wakulima mahali walipo ili waweze kununua kwa bei nafuu na hata kukopeshwa ili zitumike katika msimu huu wa kilimo ikiwa ni maelekezo ya serikali.

Kikao hiki cha kuwasilisha taarifa ya mapitio ya mwaka 2020-2021, mwenendo wa bajeti ya mwaka 2021-2022 na mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kimehudhuriwa na wajumbe mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Manyoni magharibi Mh.Yahaya Masere, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni Bw.Jumanne Ismail Makanda,Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya,Madiwani ,Wakuu wa idara  na wataalam  kutoka Halmashauri ya Wiaya ya Manyoni.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa