• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

NAIBU WAZIRI WA MADINI MH DOTTO BITEKO ASIKITISHWA NA MAKAMPUNI YANAYOCHIMBA JASI KUTOKUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA ITIGI

Tarehe ya Kuwekwa: November 20th, 2018

Naibu Waziri wa Madini Mh Dotto Samweli Biteko amesikitishwa na  Makampuni yanayojishughulisha na  Uchimbaji wa Madini ya Jasi katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kutokuchangia Miradi ya Maendeleo katika maeneo ambayo shughuli za Uchimbaji zinafanyika hasa katika kata husika na Vijiji ambavyo Madini ya Jasi yanapatikana

Hatua hiyo inatokana na Mh Ally Minja ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi kumueleza kwa masikitiko makubwa Mh Naibu Waziri  Kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi ndio Inaongoza kuwa na Madini bora ya Jasi ambayo Viwanda vingi vinapata Madini haya kwa ajili ya Utengenezaji wa saruji ikiwemo kiwanda cha Dangote. Minja alisema pamoja kuwa Makampuni Mengi lakini Makampuni haya yamekuwa hayashiriki shughuli za Maendeleo wala kutoa chochote katika Miradi ya Maendeleo ambayo inatekelezwa katika Maeneo Mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

Minja pia alimweleza Mh Naibu Waziri kuwa pamoja na kuwa Makampuni haya hayachangii Miradi ya Maendeleo pia yamekuwa yakiwadhulumu stahiki zao Vibarua wanaotumia nguvu zao kwa ajili ya uchimbaji pamoja na upakiaji wa madini hayo kwa kutokuwapa stahiki zao kwa wakati au kuwadhulumu kabisa

Minja pia alimweleza mh Naibu Waziri kuwa pamoja na Halmashauri kuwa na Madini Mengi ya Jasi bado halmashauri haipati mapato ya kutosha kwa kuwa Makampuni yanadai hayalipwi pindi wanapopeleka Jasi viwandani

Mh Naibu Waziri Dotto Biteko katika kuhakikisha vibarua wanapata stahiki zao alichukua hatua za kumtaka mmiliki wa kampuni ya GBES COMP LIMITED bwana Yusuph Kibira anawalipa vibarua  mapema iwezekavyo vinginevyo Mitambo yake itasimama na kutaifishwa mpaka pale Vibarua wote watakapo kuwa wamelipwa.

Biteko aliwataka wamiliki wa makampuni ya Uchimbaji wa madini ya Jasi kuzingatia Utunzaji wa Mazingira na endapo watashindwa kutunza mazingira hayo sheria ya Madini inasema wazi kuwa wanapaswa kufutiwa leseni zao

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Ndugu Pius Shija Luhende alisema kuwa halmshauri ya Wilaya ya Itigi itaendelea kutoa Msaada wa kisheria kama ilivyotoa kwa Charles Maige ambae amedhulumiwa stahiki yake kwa Muda Mrefu. Halmashauri haitakuwa tayari kuona Wananchi wanadhulumiwa haki zao.  Luhende Aliwataka Wananchi kuleta malalamiko ofisini kwake ili waweze kusaidiwa na kupata haki zao ambazo wanazipoteza kwa Kutishwa ama kucheleweshewa.

Abdul Jamal Mchimbaji wa Madini ya Jasi akimweleza Jambo Mh Naibu Waziri wa Madini Mh Dotto Biteko 


Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa