• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

Tarehe ya Kuwekwa: July 28th, 2022


Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa wapya, kuwahamisha vituo vya kazi waliokuwepo, huku akiwatema tisa akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi.

Uteuzi huo umetangaza leo Alhamisi Julai 28, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus

Taarifa hiyo imewataja wakuu wa mikoa wapya ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha, Nurdin Babu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Fatma Mwasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Rais Samia pia amemteua Halima Dendego kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Raphael Chegeni ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Peter Serukamba ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Pia Rais amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, mkoani Pwani, Kanali Ahmed Ahmed kuwa Mkuu wa Mkoa Mtwara, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Taarifa hiyo imeeleza Rais Samia amemteua Albert Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dk Yahaya Nawanda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Waliohamishwa

Taarifa hiyo imeeleza wakuu wa mikoa waliohamishwa vitu vya kazi ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthon Mtaka amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa Rukwa.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Waziri Kindamba amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, pia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigella amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Wanaoendelea na vitu vya kazi

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Rais Samia amewabakiza wakuu wa mikoa 10 kubaki kwenye vituo vyao vya kazi akiwemo Amos Makalla Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Batilda Burian na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge.

Wakuu wa mikoa walioachwa

Rais Samia amewatema wakuu wa mikoa tisa akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Binilith Mahenge na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joseph Mkirikiti

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa