• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

RAS MGANGA ATOA MAAGIZO

Tarehe ya Kuwekwa: May 12th, 2023

Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Bi .Fatma Mganga amesema namna bora ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendendeleo katika halmashauri ni kusimamia miradi hiyo kikamilifu ili iweze kukamilika kwa wakati na kwa viwango ili iweze kuleta tija kwa wananchi.

Akizungumza katika kikao cha robo ya tatu ya  baraza la Madiwani katika halmashauri ya Itigi RAS  amesema hakuna sababu ya miradi kushindwa kukamilika kwa wakati kwa kuwa serikali imetoa fedha za kutosha kukamilisha miradi hiyo.

Aidha ameishauri Kamati ya Fedha ,Uongozi na Mipango kuwa na Ajenda ya kupata na kujadili taarifa za miradi mbalimbali inayotekelezwa katika halmashauri kwa kila kikao ili kubaini ikiwa kuna changamoto na kuzitafutia majibu ili miradi hiyo iendelee na kukamilika kwa wakati.

Pia RAS Mganga ameitaka halmashauri kuongeza bidii katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo la asilimia 95 huku akisisitiza kuwa hali hiyo itasaidia halmashauri kujiendesha “ heshima ya halmashauri ni mapato”alisisitiza.

Katika hatua nyingine RAS ameitaka halmashauri kupitia kamati ya Elimu,Afya na Maji kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha wanalima katika mashamba ya shule zao ili kuzalisha mazao yatakayo wawezesha kupata chakula chakula

Naye Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemilembe Lwota  ameipongeza halmashauri ya Itigi kwa kubuni na kuanzisha vyanzo vipya mapato ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Maegesho ya malori katika mji wa Itigi pamoja na stendi ya magari katika Kta ya Mitundu.

Pia amewakumbusha wajumbe kuanza kujiandaa kwa ajili ya mapokezi ya Mbio za mwenge wa Uhuru mnamo mwezi septemba ikiwa ni pamoja na kuhakikisha miradi yote ambayo mbio za mwenge zitapita kukagua inakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi Mhe. Hussein Simba ameishukuru serikali inayoongozwa na Mhe,Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuipatia halmashauri hiyo fedha nyigi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi mkubwa wa Hospitali ya wilaya ,miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami,miradi ya maji na hata elimu.

Mwisho;

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa