• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

RC SINGIDA AITISHA KIKAO KUNUSURU MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI ITAGATA ITIGI

Posted on: September 21st, 2021

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge ameagiza uongozi wa wilaya ya Itigi kuitisha kikao cha viongozi wa Kijiji cha Itagata, wananchi na wadau wa kilimo ili kunusuru mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa kijiji hicho ambao Serikali ilitoa Sh. 2 Bilioni kwa ajili ya kuanzisha mradi huo ulioridhiwa na wananchi lakini haufanyi kazi kwa sababu mbalimbali.

 

Dkt.Mahenge alitoa agizo hilo jana wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na kuzungumza na wananchi.

” Ninaagiza muitishe kikao hicho haraka sana na mimi mwenyewe nitakuja, nilipokuwa nasikiliza takwimu za mradi huu za Sh.2.1  Bilioni za ambao haufanyi kazi nimesikitika sana  kwani kuna maeneo wanalia kukosa fursa ya namna hiyo nawaambia kwa uvivu wenu huo mtaendelea kulalamika na kuwa maskini “. alisema Mahenge.

Alisema baada ya kikao hicho ndipo watakapoamua kuona cha kufanya ikiwa ni pamoja na kuwapatia mashamba hayo watu wengine wenye uwezo ya kuyaendeleza baada ya wananchi wanachama wa kilimo cha umwagiliaji waliopewa kushindwa kuyafanyia kazi.

Afisa Kilimo Wilaya ya Itigi Mkinguzi Mgalula akitoa taarifa ya mradi huo kwa mkuu wa mkoa alisema mradi wa kilimo cha umwagiliaji Itagata una jumla la eneo la  hekta 160 linalofaa kwa kilimo sawa na ekari 400 na kuwa eneo linalofikiwa na miundombinu ya umwagiliaji ni hekta 83.6 sawa na ekari 209.

Alisema mradi huo ni matokeo ya wazo lililobuniwa na wananchi wa kijiji hicho wakati wa zoezi la kubaini fursa na vikwazo vya maendeleo na hatimaye kuingizwa kwenye mpango wa maendeleo ya kilimo cha Kijiji cha Itagata mwaka 2008/ 2009.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu mradi huo ambao umekwaka kuendelea viongozi mbalimbali wananchi na wadau wengine waliunga mkono agizo la mkuu wa mkoa la kuitisha kikao hicho ili kitoe maamuzi ya kuyachukua mashamba hayo na kuwapa watu wengine ambao watakuwa na uwezo ya kuyaendeleza.

Baadhi ya viongozi waliotoa maoni hayo ni pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Itagata Salum Mbesi, Diwani wa Kata hiyo Martin Kapona, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Wilaya ya Manyoni Jumanne Muhanda, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo pamoja na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho akiwepo Makamo Mwenyekiti wa Umoja wa Kilimo hicho cha umwagiliaji Itagata, Rashid Mfaume, Zena Matonya na Mussa Lupia.

Walitaja baadhi ya sababu  za mradi huo kukwama ni uvivu, ubinafsi na watu kukumbatia mashamba ambayo wanashindwa kuyaendeleza huku wengine wakiyakodisha kwa bei kubwa.

Mussa Lupia alisema Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itoa kipaumbele kwa kuwapa kwanza mashamba wananchi wa kijiji hicho walioibua mradi huo lakini wameshindwa kuyaendeleza hivyo analiunga mkono wazo la mkuu wa mkoa la kuitisha kikao hicho ili kitoe maamuzi ya kuwapa watu wengine watakaokuwa na uwezo wa kuyaendeleza kutoka ndani ya kijiji hicho na nje.

Katika ziara hiyo Dkt.Mahenge alitembelea Hospitali ya St Gaspar iliyopo Itigi mjini na kuona huduma kubwa za matibabu zonazofanyika zikiwemo za upasuaji na akatoa wito kwa wananchi mbalimbali kutoka mikoa jirani na Singida kwenda kupata huduma za upasuaji na matibabu mengine badala ya kukimbilia Hospitali zingine kubwa za hapa nchini na kutumia gharama kubwa ambapo pia alizungumza na Viongozi na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na kusisitiza ukusanyaji wa mapato na kutenga asilimia 10 ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.