• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

RC SINGIDA AWAAGIZA WAKURUGENZI NA WAKUU WA WILAYA KUSIMAMIA KWA NGUVU ZOTE MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA UKUSANYAJI WA MAPATO (LGRCIS) ILI KUONGEZA MAKUSANYO NA KUONDOA MIANYA YA UPOTEVU WA MAPATO

Posted on: September 1st, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wapili kushoto) akifungua Kikao cha Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu  Mapato na matumizi ya Halmashauri za mkoa wa Singida kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Dkt. Nchimbi amewataka watendaji, viongozi pamoja na watumishi mkoani Singida kuwa mkakati unaoonekana na kuondokana na utendaji kazi wa mazoea na kuwataka watumishi wa halmashauri kuwa na ubunifu unaozihirika ikiwa ni pamoja na kusimamia na kuendeleza ubunifu unaotolewa na baadhi ya viongozi. 




Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akiwasilisha agenda ya Tathimini ya Mapato ya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa mbele ya Wajumbe wakati wa kikao kilichoongozwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.


Katibu Tawala amewasisitiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Mkoa wa Singida kuhakikisha wanaingia kwenye Mfumo wa Mapato (LGRCIS) mara kwa mara na kuhakikisha mashine zote zinazokusanya mapato 'POS' zinaonekana kwenye 'Dashboard' ya Mfumo wa LGRCIS.

 Afisa TEHAMA wa Sekretarieti ya Mkoa wa Singida, Bw. Baraka E. Mhembano akifanya wasilisho juu ya Mfumo wa Mapato - LGRCIS unavyo fanya kazi pamoja na hali ya ukusanyaji wa Mapato katika kila halmashauri mkoani Singida,wakati wa kikao hicho kilichoongozwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Singida. 


Katika kikao hiki muhimu Wajumbe walipitishwa katika Mfumo wa LGRCIS kwa kila Halmashauri na kuona Mashine za kukusanya mapato zinavyoonekana kwenye Mfumo wa LGRCIS, pia  walioneshwa kila Mashine ni lini kwa mara ya mwisho imetuma taarifa zake kwenye mfumo Mkuu.



 Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Singida (mbele) pamoja na wajumbe kutoka halmashauri mbalimbali pamoja na taasisi mbalimbali wakifuatilia kikao cha Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na matumizi ya Halmashauri za mkoa wa Singida kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida.


 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kulia akizungumza jambo kwa msisitizo   wakati wa Kikao cha Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na  matumizi ya Halmashauri za mkoa wa Singida, kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Singida. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa Singida Dkt. Angelina Lutambi.


 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Mbua Chima (wakatikati) pamoja na Wajumbe wengine wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao hicho.


 Waheshimiwa Wenyeviti wa Halmashauri za wilaya za mkoa wa Singida (mbele) pamoja na Wajumbe wengine wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao hicho.

 Kikao kikiendelea.

 

  Kikao kikiendelea.

  Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya mkoani Singida wakiwa wanafuatilia kikao kwa makini.

  Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisisitiza jambo wakati wa kikao.

 Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Bi. Mwajabu Nyamkomola akizungumza wakati wa kikao.

 Mjumbe akichangia mada wakati wa kikao.


 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mheshimiwa Miraji J. Mtaturu (kulia) akizungumza wakati wa Kikao cha Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na matumizi ya Halmashauri za mkoa wa Singida kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Singida Vijijini mkoani Singida. 


Aidha Mhe. Mtaturu ametoa wito kwa watumishi kuwa na ushirikiano wa pamoja kati ya halmashauri na halmashauri kwa kuwa na mkakati mahususi wa mawasiliano ili kuwahudumia Wananchi  wa mkoa wa Singida kwa pamoja.

 Mganga Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Victoria Ludovick akiwasilisha Mada ya Hali ya Ujenzi wa Vituo vya Afya wakati wa kikao hicho kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Singida.



 Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza na Wajumbe wakati wa kikao.


 Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akisisitiza jambo kwa Wajumbe wakati wa kikao.


 Uwasilishwaji wa Mada ukiendelea.


   Uwasilishwaji wa Mada ukiendelea.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akionesha Mfumo wa Mapato - LGRCIS unavyofanya kazi  na kuwaagiza Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa Mapato katika Halmashauri zao.

 Kikao kikiendelea

 Katibu Tawala Mkoa Singida akifafanua jamba juu ya Mfumo wa Mapato - LGRCIS wakati wa kikao.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini Bw. Elia Digha akizungumza wakati wa kikao.

 Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Pasacas Muragiri akizungumza wakati wa kikao.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wapili kushoto) wakati akihairisha Kikao cha Kusimamia, Kudhibiti na Kuratibu Mapato na matumizi ya Halmashauri za mkoa wa Singida kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Singida Vijijini mkoani Singida.

Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.