• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

RC SINGIDA : TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA MASHIRIKA YA KIDINI ILI KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIJAMII

Tarehe ya Kuwekwa: May 14th, 2024




















Serikali ya Mkoa wa Singida imewahakishia Wadau wa Maendeleo ikiwemo Uongozi wa Hospitali ya Mtakatifu Gaspar ya Halmashauri ya Itigi Wilayani Manyoni kuwa itaendelea kudumisha ushirikiano uliotukuka katika shughuli mbalimbali wanazofanya ikiwemo utoaji wa huduma bora za msingi na za kibingwa za afya kwa wananchi wa mkoa huo.

Mkuu wa mkoa wa Singida Mheshiiwa Halima Dendego, ametoa kauli hiyo (tarehe 14/May/2024) wakati anazungumza katika maadhimisho ya Miaka 35 ya Hospitali ya Mtakatifu Gaspar Itigi.

Halima Dendego, amesema amefurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Viongozi na Watendaji wa Hospitali hiyo katika utoaji wa huduma za kiwango cha juu za afya ikiwemo mama na mtoto pamoja na uboreshaji majengo na vifaa tiba.

“Baraka na mkono wa Mungu uwe pamoja nasi na tuendelee kumwomba ili aendelee kutubariki zaidi ya hapa, Mhe. Halima Dendego.

Mkuu wa mkoa huyo amesema yeye na Watendaji wake wataendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha mashirika yenye nia njema ya kuwaletea maendeleo ya uhakika wananchi wa mkoani Singida yanafikia malengo yao kwa kutoa huduma zao bila usumbufu wowote.

Aidha amesisitiza Viongozi wa Hospitali ya Matakatifu Gaspar Itigi kama wanachangamoto yoyote ambayo inaweza kusababisha kudumaza au kuchelewesha utoaji wa huduma za afya kwenye Hospitali hiyo wamweleze ili aweze kuzitafutia majawabu haraka iwezekanavyo ili wananchi waendelee kupata huduma bora za kisasa za afya.

Naye, Mkurugenzi wa Hospitali na Chuo cha Mtakatifu Gaspar Itigi Padre Justin Boniface, ameeleza kuwa mafanikio waliyoyapata katika utoaji wa huduma za msingi na za kibingwa za afya ni kwa sababu na ushirikiano mkubwa na karibu wanaoupata kutoka Serikalini.

Amesema mkakati wao ni kuhakikisha kuwa Hospitali ya Mtakatifu Gaspar ambayo kwa sasa inahudumia wagonjwa wengi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Singida na nje ya mkoa huo inakuwa bora katika utoaji wa matibabu ya kisasa nchini ambapo kwa sasa wameanza ujenzi wa kitengo cha kusafisha damu kwa sababu ya uhitaji mkubwa wa wananchi.







Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa