• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI-WANAWAKE CHANGAMKIENI FURSA

Posted on: March 8th, 2022

Wanawake wametakiwa kushiriki katika fursa mbalimbali za kiuchumi,kisiasa na kijamii ili kuwa mfano bora katika familia zao na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Rahabu Mwagisa katika maadhimisho ya SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ambayo kiwilaya imefanyika katika hamashauri ya Itigi.

Mhe. Rahabu amesema kuwa wamawake wanapaswa kutambua sehemu ya majukumu yao katika familia na jamii kwa ujumla kwa kushiriki katika kazi mbalimbali za kiuchumi sambamba na kushiriki katika masuala ya kisiasa kwa kuwa wanawake wanauwezo mkubwa wa kutimiza majukumu hata katika ngazi ya juu ya uongozi”kwa kuwa wanawake ni jeshi kubwa hivyo ni lazima tuchangamkie fursa mbalimbali za kiuchumi,kisiasa na nyinginezo katika maeneo yetu”amesema Bi.Rahabu

Pia amewasisitiza wanawake kuwa mstari wa mbele kuwasaidia watoto wao hasa wakike kuwa na maadili mema na kuzingatia masomo ili waweze kufanikiwa katika maisha yao”wafundisheni watoto wenu hasa wakike kuwa na maadili mema na kuzingatia masomo ili kuepuka kupata mimba za mapema na kukatisha ndoto zao”amesema Bi. Rahabu

Aidha Bi. Rahabu amewataka wanawake na akina mama kuhudhuria katika vituo vya kutolea huduma za afya mapema wanapopata ujauzito ili kuepuka matatizo yanayotokana na ujauzito kwa kupatiwa huduma zinazofaa kwa wakati.

Awali akisoma taarifa kwa mgeni rasmi Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii,halmashauri ya Itigi Bi. Suzan Mushi ameseka takwimu zinaonesha kuwa  mwaka 2019 hadi 2021 wanafunzi wa shule za sekondari katika halmashauri ya Itigi waliopata mimba ni 29 wakati kwa shule za msingi kwa mwaka 2020 hadi 2021 walikua wanne.

Aidha Mkoa wa Singida unashika nafasi ya pili kitaifa  katika suala ukeketaji nyuma ya mkoa wa Manyara na Wilaya ya Manyoni na Itigi zikiongoza kimkoa”mila potofu zimepelekea mkoawa Singida kushika nafasi ya pili kitaifa ikiongozwa na mkoa wa Manyara na kimkoa  Wilaya ya Manyoni na Itigi zinaongoza katika suala hilo”.

Naye Diwani wa Kata ya Itigi Tambukareli Mh. Rehema Chizumi amewahimiza wakaazi wa halmashauri hiyo kujitokeza na kushirika kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika mapema mwezi agosti mwaka huu”jamii inapaswa kujitokeza kuhesabiwa ili serikali iweze kupata takwimu sahihi za watu na makazi”.

Maadhimisho ya siku ya wanawake hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 8 machi na kaulimbiu ya mwaka huu ni KIZAZI CHA HAKI NA USAWA KWA MAENDELEO ENDELEVU TUJITOKEZE KUHESABIWA ambapo yalienda sambamba na huduma mbalimbali za kiafya kama upimaji wa magonjwa ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake pamoja na uchangiaji damu.

Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.