• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

TARURA; BILIONI 2.1 KUJENGA MIUNDOMBINU YA BARABARA HALMASHAURI YA ITIGI

Tarehe ya Kuwekwa: January 28th, 2022

                    TARURA: BILIONI 2.1 KUJENGA BARABARA HALMASHAURI YA ITIGI.

Serikali imepanga kufanya matengenezo ya barabara na madaraja katika Halmashauri ya Itigi kupitia Wakala wa barabara Vijijini na mijini(TARURA) kwa kiasi zaidi ya  Tsh  bilioni mbili (2,138,970,000.00) kwa mwaka wa fedha 2022/2023,

Mpago wa matengenezo wa barabara na madaraja  unajumuisha matengenezo ya kawaida,Kuimarisha sehemu korofi,Matengenezo ya muda maalumu, Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami,Ufunguzi wa barabara mpya na ujenzi wa madaraja.

Hayo yamesemwa  na Mhandisi Yose Mushi kutoka Wilaya ya Manyoni,katika kikao cha kuwasilisha MAPENDEKEZO YA MPANGO WA BAJETI WA MATENGENEZO YA BARABARA NA MADARAJA  KATIKA HALMASHAURI YA ITIGI WILAYA YA MANYONI,kilicho fanyika katika Ukumbi wa mikutano katika ofisi ya Halmashauri ya Itigi na kuongeza kuwa mpango huo wa matengenezo ya barabara umegawanyika katika sehemu kuu mbili ikiwa ni Mpango wenye ukomo pamoja na mpango wa bajeti isiyokuwa na ukomo ambayo ilipendekezwa na Madiwani kwa kuzingatia vipaumbele.

Mbunge wa Jimbo la Manyoni magharibi Mh.Yahaya Masere amesema serikali imedhamiria kuunganisha Mkoa wa singida na mikoa mingine ukiwemo mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa kujenga barabara za kiwango cha lami na tayari serikali imeshatenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo katika Halmashauri ya Itigi utakaohusisha matengenezo ya barabara za TARURA pamoja na TANROADS.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi Mh.Hussein Simba ameipongeza serikali kwa kuiongezea Halmashauri yake bajeti kutoka shilingi milioni mia sita hamsini na nane (658 mil) hadi kufikia bilioni mbili (2.1 bil) kwa ajili ya kujenga miundombinu ya barabara yenye mtandao wa takribani kilometa 892.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni Bw.Jumanne Ismail Makanda amewataka wakurugenzi na watumishi wengine kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na maelekezo kutoka serikalini  na kuepuka kuingiza siasa katika utendaji  na kusababisha kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati.

Akihitimisha mjadala wa kikao hicho cha kuwasilisha mapendekezo ya mpango wa bajeti wa matengenezo ya barabara na madaraja,Mkurugenzi wa halmashauri ya itigi  Mh.John Mgalula amesema kuwa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi  inatokana makusanyo ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na TOZO  na kuwasisitiza watumishi katika halmashauri yake  kununua magari na kupiga simu kwa wingi ili serikali iweze kukusanya Tozo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa