• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

TASAF KIPINDI CHA PILI AWAMU YA TATU HALMASHAURI YA ITIGI YAANZA NA UHAKIKI WA KAYA

Tarehe ya Kuwekwa: August 1st, 2020

Uwajibikaji na uadilifu kwa wataalamu ni muhimu katika kusimamia zoezi la uhakiki wa Walengwa wa kaya maskini TASAF ambao  utasaidia kupata Takwimu sahihi  za wanufaika Halisi  ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.

Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji TASAF Bi. Ester Kivuyo katika mafunzo ya Maafisa Wawezeshaji yanayohusu Utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu TASAF yaliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

Kivuyo  alisema, Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wa kiutendaji katika kusimamia Uhakiki wa kaya maskini utakaofanyika mara baada ya mafunzo hayo ili kupata Takwimu HALISI za  Walengwa HALISI ambao wamefariki (ambao walikuwa ni kaya ya mtu mmoja asiye na mtegemezi, kaya ambayo imehama, kaya ya Kiongozi wa Kijiji, kaya ya mjumbe wa Kamati ya Usimamizi ya Jamii (CMC), kaya ambayo haikufika kuchukua malipo yake  mara mbili mfululizo. Takwimu hizo zitakusanywa kwa njia ya DODOSO, na kuingizwa kwenye Mfumo wa Takwimu.

Alisema “Halmashauri ya Wilaya ya Itigi ina wanufaika  wa TASAF  3,519, kwa vijiji 39 katika kata 13 zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi ambazo zinapata huduma ya TASAF. Aliongeza kuwa Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini pia umewezesha kaya za walengwa kujikita kwenye shughuli za kukuza kipato na kujiimarisha kiuchumi ikiwemo ufugaji, uvuvi, kilimo na biashara ndogo ndogo.

 Hata hivyo kivuyo alianisha  baadhi ya kaya za  wananchi wanaoishi katika hali duni kwenye maeneo ambayo hayakufikiwa, Hivyo Kipindi cha Pili katika Awamu ya Tatu ya TASAF  kaya zote zinazoishi katika mazingira duni zipate usaidizi wa Serikali kupitia TASAF kwa kuwawezesha kufanya kazi na kupambana na umaskini.”

 Aliongeza kuwa, Mkazo mkubwa katika Kipindi cha Pili utawekwa katika kuwezesha Kaya zitakazoandikishwa kwenye Mpango kufanya kazi ili kuongeza kipato na kuhakikisha kwamba huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa  na kuendeleza rasilimali watoto hususani katika upatikanaji wa elimu na afya. 

 Aliwasisitiza  Viongozi hao kufanya kazi kwa uadilifu na weredi wakati wa utekelezaji wa Zoezi hili  kama maagizo yaliivyotolewa na Mh Rais katika hotuba  yake wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Pili kuhusu uwepo wa kaya hewa. “Nanukuu. “ Uwepo wa kaya hewa katika maeneo ya utekelezaji ni aibu sana kwa viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri. Nitoe wito kwa wahusika wote kusimamia vizuri mradi huu. Serikali haitakuwa na huruma kwa mtu yeyote. Kufanikiwa ama kutofanikiwa kwenye maeneo yenu itakuwa mojawapo ya vipimo nitakavyotumia kujua kama mnastahili kuendelea na nafasi mlizonazo au la. Siwatishi lakini huo ndio ukweli” mwisho wa kunukuu.

Bi Ester Kivuyo kwa kuhitimisha aliwakumbusha wananchi wote kuchukua tahadhari ya ugonjwa hatari wa COVID-19  ili   kuepuka Mikusanyiko isiyoyalazima, kuvaa barakoa,  kuepuka kushikana  mikono na  kunawa mikono kwa sabuni kwa kutumia maji safi yanayotiririka pamoja na kutumia vitakasa mikono. 

Mratibu wa Mradi wa Tasaf  Halmashauri ya Itigi ndugu Valence Kilasara (Kushoto) Akikabidhi Kishikwambi kwa Afisa Mwezeshaji Bi Haidai Magoma kwa ajili ya Uhakiki wa Kaya


Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa