• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

TUMIENI FURSA ZA MRADI WA RELI YA SGR KUINUA UCHUMI-Prof. Kahyarara Katibu Mkuu Uchukuzi

Tarehe ya Kuwekwa: May 15th, 2024

Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Walter Kahyarara amewataka Wakazi wa Itigi Wilayani Manyoni Mkoani Singida kuwekeza katika Kilimo cha mazao ya chakula, Mbogamboga na Matunda na ufugaji wa kisasa kutokana na fursa ya mradi wa reli ya Mwendokasi ya kisasa (SGR) unaopita katika Mji wa Itigi kutoka Jijini Dar es Slaam Kuelekea Jijini Mwanza na nchi Jirani.

Prof Kahyarara amesema hayo Katika ziara yake ya kuzungumza na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kueleza fursa za kiuchumi zinzazotokana na mradi huo akiwa ameambatana na Wataalam Kutoka Wizara ya Uchukuzi, Shirikia la Reli Tanzania (TRC), Chuo Kikuu Cha Sokoine Morogoro (SUA) na Tasisi ya TanChoice Limited

Aidha ,Prof Kahyarara amesema, Serikali inaagiza mabehewa ya mizigo  yakiwa na uwezo wa kutunza ubora wa bidhaa (cold rooms) na wanajenga maghala yenye uwezo wa kutunza bidhaa (Cold rooms)  katika bandari zitakzotumika kusafirisha mizgo kwenda katika masoko duniani kote   

Prof Kahyarara amemsisitiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kuhamasisha wakulima na wafugaji kuwekeza kisasa na kupata mazao mengi ambayo watauza katika masoko ya kimataifa kwakuwa reli itakuwa ni usafiri wa uhakika , haraka na utatunza na kusafirisha bidhaa kwa ubora uleule

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Huduma  wa shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Makoye Sahani amesema Reli hiyo inatarajiwa kusafirisha mizigo mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa maroli 500 ya mizigo na inatarajiwa kutembea kwa spidi ya KM 120 kwa saa.

Aidha Sahan alisema kukamilka kwa reli hiyo kutachochea maendeleo katika sekta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususani katika maeneo ambapo reli hiyo inapita na kwa nchi jirani hasa Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na Kongo DRC

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Ayoub Kambi alisema, Halmashauri kupitia wataalam wa Kilimo , Mifugo , biashara na ardhi wameanza kutoa elimu kwa wananchi  ili waweze kuwekeza katika mazao ya kimkakati kwa kuzingatia mahitaji ya soko

Hata hvyo Kambi, alimuelesza Katibu Mkuu kuwa kuna eneo lenye ukubwa wa hekta elfu 45 la Tanganyika Peckers katika kata ya Kiataraka ambalo lina mgogoro wa uvamizi wa wananchi ambalo linauwezo wa kuchangia uwekezaji wa mifugo na kilimo.

Hata hivyo, Kambi alisema,  jitihada za kutatua mgogoro huo zinaendelea kwa kushirikisha wananchi, Wizara ya Mifugo na Idara mbalimbali za Serikali kufikia suluhu ya mgogoro huo ili eneo hilo lianze kutumika kwa uwekezaji..

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa