• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Atembelea Msitu wa Itigi 'ITIGI THICKETS'

Tarehe ya Kuwekwa: August 19th, 2018

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa, January Makamba jana  alihitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Singida na kuwasili katika Mkoa wa Tabora, ikiwa ni mwendelezo wa kukagua, kutathmini, kuzungumza na viongozi, na wananchi kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira, sambamba na uanzishwaji na ufuatiliaji utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi Mazingira ya mwaka 2004 katika ngazi za Serikali za Mitaa.

 

 

Katika siku ya tatu ya ziara yake Mhe. Makamba ametembelea vichaka vya Itigi ‘Itigi thicket” na kupata fursa ya kuzungumza na viongozi wa wilaya ya Manyoni juu ya namna bora ya kuhifadhi eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 410,000 na kuahidi kutuma wataalamu kuandaa andiko la Mradi utakaonufaisha wakazi wa eneo hilo katika sekta uvunaji wa asali kwa njia ya kisasa zaidi.

 

 

“Ndani ya muda mfupi nitatuma wataalamu wangu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, waje wakae na wataalamu wenu na kuandaa Mradi utaonufaisha wakazi wa wanaozunguka eneo lote la msitu ili kutunza na kuhifadhi rasilimali za asili zilizopo katika eneo hili” Makamba alisisitiza.

 

 

Katika hatua nyingine Waziri Makamba amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Bi. Rahabu Jackson kuwasilisha kwake majina wa watalaamu wa Mazingira ambao wana sifa za kuwa Wakaguzi wa Mazingira ili waweze kuteuliwa kwa mujibu wa Sheria.

Pia, ametoa wito wa Halmashauri kuingia makubaliano na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kukasimu mamlaka kisheria ya kukagua na kusimamia masuala ya mazingira kwa msukumo zaidi

Vichaka vya Itigi huwa na urefu wa mita 2-5 na katika Bara la Afrika vinapatikana Tanzania na Zambia pekee vinawakilisha bioanuani ya kipekee duniani yenye umuhimu kitaifa na kimataifa na uoto wake ni  muhimu kwa mustakabali wa maisha ya binadamu na wanyamapori.

Imebainika kuwa vichaka vya Itigi viko hatarini kutoweka kutokana na shughuli za kibinadamu kama vile kilimo cha kuhamahama, uchungaji wa mifugo, uchomaji wa mkaa, uvunaji wa mazao ya misitu na uchimbaji wa madini. Hivyo kuna haja ya kuchukua hatua za haraka kuhakikisha uhifadhi endelevu wa vichaka vya Itigi.

Makamba akimsikiliza mmoja wa wananchi wa eneo hilo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akisalimiana na Bw. Khatib Ally mmoja wa wananchi waliojitokeza kumpokea katika Kijiji cha Aghondi Wilayani Manyoni, Mkoani Singida. Waziri Makamba ametembelea eneo hilo ambalo lina vichaka vya aina yake na vyakipekee barani Afrika. 


Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa