• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

WADAU WA AFYA HALMASHAURI YA ITIGI WAHIMIZWA KUCHAPA KAZI KWA WELEDI

Tarehe ya Kuwekwa: June 15th, 2022


Wadau wa afya katika halmashauri ya Itigi wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ili kuisaidia Serikali kutekeleza Mkataba wa Utendaji kazi na usimamizi wa shughuli za Lishe nchini.

Akizungumza katika kikao kazi cha kuhuisha mkataba wa Lishe na Tamko la Jiongeze Tuwavushe Salama Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Bi. Rahabu Mwagisa amewataka Waganga wafawidhi wa vituo vya afya na watendaj wa Kata katika halmashauri hiyo kutambua kuwa serikali imefanya jambo kubwa kwa kuingia mkataba huo na kuwataka  kutekeleza maagizo wanayo pewa na serikali ili mkataba huo uweze kuleta tija.

Mkuu huyo wa Wilaya amesikitishwa na baadhi ya waganga wafawidhi pamoja na watendaji wa Kata kushindwa kuwasilisha ripoti za utendaji kazi kwa wakati na kuwasisitiza kufanya hivyo ili kuunga mkono jitihada za  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia mhesimiwa Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza majukumu yake kwa upande wa sekta ya afya.

Mkurugenzi Mtenadaji wa halmashauri ya Itigi Bwana John Mgalula amemuagiza Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo kumpelekea  barua  ya wanganga wafawidhi wote walioshindwa kuwasilisha ripoti zao kwa wakati na kusababisha halmashauri kuonekana kushindwa kutimiza matakwa ya mkataba huo.

Awali akitoa taarifa ya mkataba wa Lishe na Tamko la Jiongeze Tuwavushe Salama awamu ya kwanza,Mganga Mkuu wa halmashauri ya Itigi,Dkt.Emmanuel Mallange amesema kuwa halmashauri imejipanga kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya Mkataba huo na kuzitaka Kata zilizoshindwa kuwasilisha taarifa kwa wakati kuona umuhimu wa kufanya hivyo huku Muuguzi Mkuu wa Halmashauri hiyo Bwana  Frederick Gaisha akitoa wito kwa Watendaji Kata kutumia majukwaa yao kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya afya na lishe.

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iliingia mkataba na Wakuu wa Mikoa ishirini na sita  wa Utendaji Kazi na Usimamizi wa Shughuli za Lishe Tanzania bara kwa awamu ya kwanza tangu Disemba 19,2017 na kufikia mwisho mnamo Juni 30,2021 na pande hizo mbili zimekubaliana kuongeza mkataba kwa kipindi cha miaka mitano hadi Juni 30, 2026.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa