• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

WAFUGAJI NYUKI HALMASHAURI YA ITIGI WAPATIWA MAFUNZO

Tarehe ya Kuwekwa: April 6th, 2022

        


Jamii imetakiwa kutumia fursa ya ufugaji wa nyuki kwa njia ya kitaalamu ili waweze kupata mazao mengi  na bora kwa lengo la  kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Utawala na Maendeleo ya rasilimaliwatu kutoka Idara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Bwana, Edward Nkembu katika mafunzo kwa wajasiriamali wanaojishughulisha na ufugaji wa nyuki katika kata za Mwamagembe,Itigi majengo na Sanjaranda katika Halmashauri ya Itigi.

Bwana Nkembu amesema kuwa mafunzo haya yamekusudiwa kuwasaidia wajasiria mali katika sekta ya nyuki kufanya shughuli zao kitaalamu ili waweze kuzalisha bidhaa  kwa wingi na zenye viwango vya ubora ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

Aidha Bw.Nkembu amesema  kuwa Idara  ya Uwekezaji ,viwanda na biashara kupitia mradi wa Enhanced Intagreted Framework(E.I.F) imepanga kuweka viwanda viwili  vya kuchakata asali pamoja na mazao yake kama nta ,maziwa ya nyuki na gundi ya nyuki katika katika kata ya Mwamagembe na Itigi majengo kutokana na maeneo hayo kuzalisha asali kwa wingi na kusisitiza kuwa mpango  huu utaongeza ajira kwa jamii “tutaweka viwanda viwili katika kata ya Mwamagembe na Itigi majengo vya kuchakata asali pamoja na mazao yake ili kuchechemua ajira pamoja na uzalishaji wenye tija katika sekta ya ufugaji wa nyuki”alisema Nkemba.

Kwa upande wake  Meneja wa SIDO  Mkoa wa Singida Bi.Agnesi Yesaya  amesema kuwa  kupitia mafunzo hayo wajasiriamali watapata maarifa  ya namna bora ya kutafuta masoko sanjari  kuhifadhi asali iliyochakatwa katika vifungashio ili kuiongezea thamani.”tunawafundisha kuongeza thamani ya mazao ya nyuki kwa  kutumia vifaa vya kisasa vya kuchakata asali na kuhifadhi katika vifungashio  bora  ili kulinda thamani ya bidhaa”amesema bi.Agnesi.

 Mkuu wa Kitengo cha Maliasili katika halmashauri ya Itigi Bwana Jonn Makotta amesema   kuwa halmashauri hiyo hukusanya mapato takribani shilingi milioni hamsini kwa mwaka kupitia tozo mbalimbali zinazotokana  na mazao ya nyuki huku akibainisha kuwa ufugaji wa nyuki una faida nyingi ikiwemo utunzaji wa mazingira.”mkifuga nyuki kisasa  mtapata mazao mengi lakini mtakuwa rafiki wa mazingira”amesema Makotta

Nao wanufaika wa mafunzo hayo Bwana Hamisi Samade wa kata ya Itigi majengo pamoja na Bi.Hadija Seif kutoka kata ya Sanjaranda wameishukuru serikali kwa kuja kuwekeza viwanda vya kuchakata asali pamoja na mazao yake katika halmashauri ya Itigi,''viwanda hivi vikikamilika vitatukomboa wajasiriamali wa ufugaji wa nyuki kwa kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja pamoja na taifa kwa ujumla'' amesema Samade.

Naye Makamu wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi amesema mradi wa ujenzi wa viwanda vya kuchakata asali katika halmashauri hiyo utakaogharimu fedha takribani milioni 150  utaleta tija kwa wafugaji wa nyuki sambamba na halmashauri kwa kuwa itaweza kukusanya tozo  kutokana na uzalishaji mkubwa wa mazao hayo ya nyuki.



Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa