• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

WAFUGAJI NYUKI ITIGI DC WAUNDA JUMUIYA

Tarehe ya Kuwekwa: January 25th, 2023

Jumuiya mpya ya Vikundi vya Wajasiria mali wa ufugaji wa nyuki katika halmashauri ya Itigi wametakiwa kuwa na ushirikiano,umoja na nia thabiti ili jumuiya hiyo iweze kupiga hatua za kimaendeleo.

Akizungumza na wanajumuiya  kutoka vikundi 23 vinavyounda jumuiya hiyo  Mkuu wa Divisheni ya Ardhi na Maliasili Ndg. John Makotta amesisitiza kuwepo kwa umoja na ushirikiano baina yao ili waweze kujisimamia wenyewe na kuifanya  jumuiya  kuwa imara  na kwamba serikali  kupitia wizara ya maliasili na  utalii ipo tayari kutoa mafunzo ya ufugaji bora wa nyuki na biashara.ya asali na mazao yake.

Amesema kuwa serikali ina nia thabiti ya kuwainua wananchi kiuchumi  kupitia shughuli mbalimbali wanazofanya katika maeneo yao na kuongeza kuwa serikali hutoa fursa nyingi kupitia jumuiya na vikundi vilivyosajiliwa rasmi.

Nae Afisa biashara  Ndg. Emmanuel Mlenge amesema kupitia kuanzishwa kwa jumuiya hiyo wanaweza kupata fursa nyingi zikiwemo urahisi wa kupata mikopo kutoka katika taasisi za kifedha sanjari na kupata soko la uhakika la bidhaa wanazozalisha.

Pia Mlenge amewakumbusha umuhimu wa kuweka taarifa na kukmbukumbu za shughuli za kila siku zinazofanywa na jumuiya ili waweze kutambua muelekeo wa biashara ili kufikia malengo huku Mwanasheria wa halmashauri ya Itigi Ndg. Gilbart  Kalanda akiitaka jumuiya kuandaa katiba ambayo itawaongoza na kuweka muelekeo na malengo ya jumuia ambayo pia kutakuwa na sheria ndogo zitakazodhibiti ubadhilifu katika biashara ya asali na mazao yake ndani ya eneo la halmashauri.

Kwa upande wake Bwana Hamisi Samade  ambaye ni mwanajumuiya  kutoka kikundi cha ufugaji wa nyuki cha Itigi ameshukuru serikali kwa kuwaunga mkono na pia anaona kuwa jumuiya hiyo  hatimaye itakuwa  taasisi kubwa ambayo itawanufaisha wanajumuiya na jamii kwa ujumla.

Kwa upande mwingine Jumuiya  imefanya uchaguzi wa viongozi kujaza nafasi mbalimbali ambapo nafasi ya Mwenyekiti wa jumuiya  imekwenda kwa Bwana Elfasi E. Lwanji na Makamu wa Mwenyekiti ni Bi. Saada Ramadhani,Katibu wa Jumuiya ni Bw. Hamisi Samade na Katibu msaidizi ni Hamisi Ali huku nafasi ya Mweka Hazina ikichukuliwa na Bi.Wanjita  Clement.

Jumuiya ya Vikundi vya Wajasiria mali wa ufugaji wa nyuki katika halmashauri ya Itigi ambayo imepewa jina la   Jumuiya ya Wafugaji wa Nyuki Muhesi inaundwa na wanachama kutoka vikundi 23 vya wafugaji wa nyuki kutoka  Itigi,Mitundu,Kayui,Doroto,Kitaraka,Sanjaranda, Mwamagembe na Rungwa.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa