• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wataalamu Halmashauri ya Wilaya ya Itigi watembelea Pori la Akiba la Rungwa Kizigo Muhesi

Tarehe ya Kuwekwa: December 28th, 2018

Waheshimiwa Madiwani  pamoja na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Mh Ally Minja Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Pius Shija Luhende imefanya ziara takribani siku 3 kutembelea pori la Akiba Rungwa, Kizigo Muhesi kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazoendelea katika pori hilo pamoja na kupata taarifa za uendeshaji wa pori hilo

Akitoa Taarifa Meneja wa Pori la Akiba Rungwa Kizigo Muhesi Patrick Kutondolana amesema kuwa mapori ya Akiba ya Rungwa/kizigo/muhesi ni mapori matatu yaliyoanzishwa kwa nyakati tofauti na hatimaye kuunganishwa kiutawala na kuendeshwa kwa pamoja kutoka makao makuu ya Rungwa

Patrick na Meneja wa Rungwa/kizigo/muhesi amesema kuwa Mapori yote haya matatu yana jumla ya kilometa za mraba 17,340(kulingana na mpango wa utekelezaji GMP)  Eneo kubwa la mapori hayo yana uoto wa asili wa miombo ya Zambezi ,Somali-Masai (Acacia commiphora na deciduous and thicket) Vilevile ni mojawapo ya maeneo yaliyotengwa Itigi “thicket” ambayo ni uoto wa asili wa kipekee hapa Tanzania

Hata hivyo Kutondalana  amesema kuwa  Mapori hayo yameunganishwa katika muundo wa kanda tatu ambazo ni Rungwa Kizigo na Muhesi  kutokana na Mpango wa utekelezaji GMP. Kanda hizo bado hazijaanza kufanya kazi kutokana na miundombinu kutokamilika katika kanda husika. Kutondolana alisema pia pori lina jumla ya vituo vya nje “Rangerpost” Saba  kati ya hivyo vituo vine vinafanya kazi ambavyo ni Mwamagembe ,Jarmono,Doroto na Nkonko Vituo viwili vya makwasa na Mpululu vipo kwenye ukarabati mkubwa

Aidha Kutondalana amesema pori la Akiba Rungwa /Kizigo/Muhesi ni Mashuhuri kwa kuingiza fedha za kigeni kupitia uwindaji wa Kitalii. Kuna Misitu ya Miombo yenye kutoa makazi na malisho muhimu kwa wanyama pori mbalimbali kama, Korongo, na pahalahal kwa wingi , Tembo , Simba, Chui, Tandala mkubwa na Mdogo,Duma, Nyati Swalapal,  Pundamilia na Jamii mbalimbali za ndege zaidi ya aina (species) 300. Simba, Chui na Nyati ni Baadhi ya  wanyamapori wanaowindwa zaidi kwa ajili ya nyara za kitalii wakifuatiwa na Pundamilia.

Katika Vitalu vya Uwindaji Kutondolana alisema kuwa pori la Rungwa /Kizigo/Muhesi lina Jumla Ya Vitalu 12 vya uwindaji hata hivyo kwa sasa vitalu 3 havijapata wawekezaji.

Akizungumza katika kuhitimisha ziara hiyo ya Siku tatu katika Pori la Akiba Rungwa/Kizigo/Muhesi  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi  Pius Shija Luhende alisema kuwa Ziara hiyo itakuwa na mafanikio makubwa katika ufuatiliaji wa Jinsi hifadhi hiyo inavyofanya kazi kwa kuwa tumeweza kuitembelea hifadhi yote na kufahamu kazi zinazofanyika pamoja na kupata idadi kamili ya vitalu vya Uwindaji ambavyo sisi kama halmashauri itatusaidia kuweza kufuatilia mapato yetu vizuri

Luhende alisema pia pamoja na kujua Mipaka ya Hifadhi hii, kazi zinazofanyika pia tutaweza kufanya kazi kama Timu ili tuweze kuwaletea wananchi maendeleo

Naye Mh Diwani wa Kata ya Rungwa Edward Machapaa alishukuru sana kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kufanyika kwa Ziara hiyo ambayo imekuwa na Mafanikio makubwa pamoja na kupata elimu mbalimbali juu ya Utunzaji wa mazingira pamoja na maisha ya wanayamapori wanavyoishi pamoja na Tabia zao mbalimbali

Aidha Machapaa alisema kuwa kumekuwa na Tatizo la Majangili kuingia kipindi cha Masika na kufanya Uharibifu wa Hifadhi yetu ivo naiomba serikali kuongeza nguvu ili tuweze kuilinda hifadhi yetu na itusaidie sisi watu wa Rungwa pamoja n Taifa kwa Ujumla .

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Itigi Mh Ally J Minja akitoa neno alisema kuwa shukrani nyingi sana kwa uongozi wa Rungwa kizigo Muhesi kwa Mapokezi haya Makubwa mliyotufanyia , mmekuwa wakarimu wakati wote wa ziara yetu tumeweza kujifunza , kuona wanyama pamoja na Maisha yao  Tunapoondoka leo Tunaondoka kwa pamoja tukiwa tunanguvu ya pamoja ya Kusimamia uhifadhi wa Pori la Akiba Rungwa Kizigo Muhesi

Aidha Minja Alisema kuwa  sisi kama viongozi tunawajibu wa Kulinda hifadhi  ili pia itusaidie upatikanaji wa Mvua za Kutosha Pamoja na Mengine mengi Meneja Uliyotuambia halmashauri ya Itigi itakuwa bega kwa bega na Wewe kuhakikisha kuwa tunalinda hifadhi zetu kwa pamoja tuatahakikisha Majangili hawapati nafasi ya Kuhujumu rasilimali hii tuliyonayo.

Waheshimiwa madiwani pamoja na wataalamu wakipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Hifadhi ya  Rungwa kizigo muhesi katika Mpaka unaotenganisha Mto Mzombe na Mto Ruaha

Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika Daraja kubwa Linalotenganisha Hifadhi ya Rungwa pamoja na Hifadhi ya Ruaha

Waheshimiwa Madiwani wakiwa kwenye Kivuko kinachotumika wakati Mto mzombe ukiwa Umejaa maji

Kiboko ni kati ya wanyama wanopatikana kwa wingi katika Mito 18 iliyopo katika Hifadhi ya Rungwa , Kizigo Muhesi

 Tembo wanyama ambao wanasadikiwa kuwa wengi sana katika hifadhi ya Rungwa Kizigo muhesi kuliko hifadhi nyingine hapa Tanzania



Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa