• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Itigi District Council
Itigi District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Itigi District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Departments/Units
      • Administration and Human Resource Management
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Animal Keeping and Fishing
      • Agriculture and Corperation
      • Engineering
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Community Development and Social Welfare
      • Land and Natural Resources
      • Environment and Cleaning
      • Water
      • Health
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Legal
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
      • Beekeeping
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Farming
    • Keeping
  • Services
    • Health
    • Water
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • List of Councilors
    • Committees
      • Finance
      • Education, Health and Water
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • AIDS
      • Maadili
    • Timetable
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Bylaws
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Videos
    • Photo Gallery
    • News
    • Press Release

WAJUMBE WA MPDSR WAIBUKA NA MAAZIMIO

Posted on: May 1st, 2023

Wajumbe wa Kikao cha kujadili vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi pamoja na watoto wachanga (MPDSR) wameazimia kufanyia kazi changamoto mbalimbali zilizoainishwa na kujadiliwa katika kikao hicho ili kuzuia  vifo vya makundi hayo mawili.

Akifunga kikao kazi kilichofanyika katika halmashauri ya Itigi,Mganga mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Victorina Ludovick amesema vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga vimeendelea kuongezeka katika Mkoa wa Singida vikichochewa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wazazi kutohudhuria kliniki au kituo cha kutolea huduma kwa wakati.

Amebainisha sababu nyingine kuwa ni pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara katika maeneo mengi hasa ya vijijini,uhaba wa dawa na vifaa katika vituo vya kutolea huduma sanjari na watoa huduma kushindwa kufanya maamuzi  sahihi ya kutoa rufaa kwa wakati.

Mganga Mkuu ameainisha takwimu za vifo vya akina mama na watoto wachanga kuwa tangu mwaka 2020 ni vifo 46 vya akina mama na 747 kwa watoto wachanga,2021 vifo 44 kwa akina mama na 681 kwa watoto na 2022 ni vifo 52 kwa akina mama na 540 kwa watoto wachanga na kusisitiza kuwa hali hii haikubaliki na kuongeza kuwa kikao kazi hicho kimewapa nafasi ya kuonyana,kukumbushana kuwajibika,kuboresha huduma na kuwa na takwimu sahihi.

Naye Muuguzi mkuu wa Mkoa wa Singida Hyasinta Alute ameshauri jamii ielimishwe juu ya umuhimu wa akina mama kuaza kliniki mapema ili waweze kupata huduna muhimu kwa wakati na kuongeza kuwa idara ya Afyamkoa imeendelea kushirikiana vizuri na mfumo wa M-MAMA ili kuokoa vifo vya akina mama na watoto wachanga.

Aidha Kiongozi wa timu ya Huduma Mkoba kutoka shirika la Marrie Stopes Bi. Flora Shirima ameseka kikao hiki kimeonesha maeneo ambayo yanahitaji kupewa kupaumbele na kuahidi kuwa ombi la kusaidia timu ya dharura ili kuokoa maisha ya makundi hayo mawili  ameyakariri na atayafikisha katika ngazi husika.

Kwa upande wake Meneja wa Damu salama Kanda ya kati Dkt. Kitura Mthias amesema Mkoa wa Singida umefanya vizuri katika ukusanyaji wa damu kwa asilimia 135.87 huku Mganga mkuu wa halmashauri ya Itigi Dkt. Emmanuel Mallange amewashukuru wajumbe kwa kushiriki vizuri katika kikao hicho na kusisitiza kuwa dhima ya kikao hicho ni kusema ukweli na kujifunza ili kuboresha mapungufu yanayojitokeza katika maeneo mbali mbali.

Announcements

  • Tangazo la kura ya Rais September 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI LABADIRISHWA JINA SASA LINATAMBULIKA KAMA "JIMBO LA ITIGI" May 12, 2025
  • View All

Latest News

  • KIKAO KAZI CHA WADAU WA AFYA KUTATHIMINI TAKWIMU NA MAOTEO YA ROBO YA NNE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25

    August 27, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ITIGI KUPIIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDG YOHANA MSITA AREJESHA FOMU YA UTEUZI WA UBUNGE

    August 27, 2025
  • TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA TAARIFA YA UKAGUZI KWA MENEJIMENT YA ITIGI DC

    August 25, 2025
  • SHIMISEMITA TANGA

    August 25, 2025
  • View All

Video

YANGA DAY
More Videos

Quick Links

  • Our Instagram
  • Our Facebook
  • TAMISEMI
  • ikulu
  • NeST
  • NECTA

Related Links

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2018 Itigi Distict Council. All rights reserved.