• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

Wananchi Halmashauri ya Itigi watakiwa kuacha kukata miti Hovyo

Tarehe ya Kuwekwa: January 23rd, 2021

Na Luganuzi Muwelu.  H/W-ITIGI

Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Ndugu John Makota Amewataka Wananchi kuacha kukata miti ovyo katika maeneo yao bila  Vibali husika vya Ukataji au Uvunaji wa Miti,

 Makota Amemuleza Mgeni rasmi  Hayo  katika maadhimisho ya Upandaji Miti kitaifa kuwa kumekuwepo pia na ongezeko la shughuli za kibinadamu zinazochangia  uchomaji moto ovyo, ukataji wa miti kwa ajili ya kilimo kisichokuwa endelevu, Ujenzi wa makazi, nishati kama vile mkaa kuni na mbao , ulishaji wa mifugo holela na hata ufahamu  mdogo wa uhifadhi Mazingira ambavyo vyote hivi kimsingi vinachochea uharibifu wa Mazingira.

Awali Makota ambaye Pia ni Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili Amesema kuwa halmashauri ya Itigi katika Msimu wa Mwaka 2020/2021 imepanga kupanda jumla ya miti 500,000, Yaani miti ya Matunda , Miti ya Mbao na Miti ya Vivuli ambayo itapandwa katika taasisi za serikali hususani kwenye Ofisi za serikali, shule za Msingi na Sekondari , Taasisi za kidini na Binafsi , Maeneo ya Wazi , Kwenye mashamba na makazi ya watu. 

Aidha Makota Amesema kuwa kwa sasa jitihada kubwa zinafanyika kuhamasisha wananchi kulima Mazao ya Muda Mrefu kama Vile Korosho na Zao la parachichi na kuzitaka kila kaya katika maeneo yao kupanda miti isiyopungua 10 kwa mwaka.

Naye Akimwakilisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh Jonathan Dulle Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Amesema kuwa ni wakati sasa umefika wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na shughuli za binadamu zinazoathiri uoto wa asili pamoja na kuchukua hatua kwa wahusika wanaojishughulisha na shughuli za uharibifu wa Mazingira

Aidha Dulle amesema kuwa mkakati wa halmashauri wa uanzishwaji wa Bustani moja ya Miche kila kata utiliwe Mkazo ili halmashauri iweze kuwa na vitalu vyake vya miti vitakavyowezesha upatikanaji wa Miti kwa urahisi

Pia dulle kabla ya uzinduzi wa  maadhimisho  hayo amezitaka idara husika pamoja na Wakala wa Misitu kutoa Elimu kwenye Jamii umuhimu wa Uhifadhi wa Misitu.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi (Kulia) ndugu Jonathani Dulle akitoa Hotuba kwa Niaba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Manyoni

Kaimu  Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya  Itigi Afisa Bwana John Makota akitoa Hotuba kwa Mgeni Rasmi

Mwenyekiti wa Kijiji cha Songambele Bwana Mlangida Akipanda Mti siku ya maadhimisho ya Upandaji Miti Kitaifa katika Halmashauri ya Itigi

Afisa Ardhi Mteule Bwana Abraham Mfwimi Akipanda Mti siku ya maadhimisho ya Upandaji Miti Kitaifa katika Halmashauri ya Itigi

Afisa Nyuki Bwana Joseph Mboya Akishiriki katika zoezi la Upandaji Miti katika Halmashauri ya Itigi

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa