• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Itigi District Council
Itigi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Maji
      • Afya
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Mji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Shera Ndogo
    • Fomu za maombi Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Taarifa kwa umma

WAUGUZI NI UTI WA MGONGO WA SEKTA YA AFYA

Tarehe ya Kuwekwa: May 28th, 2022

Serikali  imewapongeza  wauguzi nchini kwa mchango wao katika sekta ya afya kwa kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi licha ya changamoto wanazokabili.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi  yaliyofanyika katika halmashauri ya Itigi mgeni rasmi Mganga mkuu wa halmashauri hiyo  Dkt.Emmanuel Mallange kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji Bwana  John  Mgalula amesema kuwa wauguzi wanafanya kazi kubwa  na kwa weledi katika kutoa huduma kwa jamii.

Daktari Mallange amesema kuwa bado kuna upungufu wa wauguzi katika sekta ya afya hususani ngazi ya halmashauri na kuwataka kuufanya kazi kwa juhudi na maarifa licha ya changamoto hizo na kuahidi kuwa baadhi ya changamoto na maombi ya wauguzi hao kufanyiwa kazi

Awali akisoma risala Muuguzi mkuu wa halmashauri ya Itigi Bwana Fredrick Gaisha  amebainisha baadhi ya changamoto zinzowakabili wauguzi ikiwa ni pamoja na upungufu wa wauguzi,gari ya idara ya afya  na sare za kazi huku akisisitiza kuwa kada ya wauguzi inachangia nguvukazi  ya idara ya afya kitaifa kwa asilimia sitini na zaidi ya asilimia themanini ya huduma zote za afya hutolewa na wauguzi.

Kwa upande wake Mratibu wa afya ya uzazi na watoto katika halmashauri ya Itigi Bi.Fortunata Simon amewapongeza wauguzi kwa kuchagua wito mwema na kuwataka kufanya kazi kwa upendo  ili kuokoa maisha ya watu huku Bwana Abdallah Kitunga  mkazi wa Itigi majengo aliyefika kupata huduma  za upimaji wa afya akiwapongeza wauguzi kwa kazi nzuri.

Maadhimisho ya siku ya wauguzi katika Halmashauri ya Itigi yameenda sambamba na utoaji bure wa huduma za upimaji ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kwa akina mama,presha ,uzito,uchunguzi wa kifua kikuu,chanjo ya UVIKO-19 na kutoa elimu ya lishe juu ya makundi matano ya chakula huku kauli mbiu ikiwa ni WAUGUZI SAUTI INAYOONGOZA,WEKEZA KWENYE UUGUZI NA HESHIMU HAKI KULINDA AFYA KWA WOTE.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA October 17, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA April 08, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI

    December 10, 2024
  • SITAKI KUONA MTU ANACHEZA NA WATOTO WA SHULE-RC DENDEGO

    November 10, 2024
  • DC MANYONI APIGA MARUFUKU UKATAJI WA VICHAKA VYA ITIGI

    November 01, 2024
  • SERIKALI KUBORESHA HALI YA WAZEE

    October 17, 2024
  • Tazama zote

Video

WALIOFAULU WARIPOTI SHULENI
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Hotuba mbalimbali
  • Taarifa mbalimbali

Tuvoti mashuhuri

  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Barabara yenye urefu wa km 10 kujengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Itigi kwa zaidi ya sh. bilioni 8 kukamilika julai mwakani
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

Kinasajii Watumiaji Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watumiaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Itigi

    Anwani ya Posta: S. L. P. 70 Itigi

    Simu: 0684483226

    Simu ya Mkononi: 0684483226

    Barua pepe: ded.itigidc@singida.go.tz

Mawasiliano Yetu

   

    • Sera ya Faragha
    • Malalamiko
    • MMM
    • Ramani

Haki miliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Itigi :Haki zote zimehifadhiwa